Matukio mbalimbali katika picha kwenye maadhimisho ya miaka 17 tangu kuanzishwa kwa huduma ya Kanisa la WRM jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kusheherekea Sikukuu ya Pasaka kwa kukumbuka mafunzo mema ya Dini.

Kauli hiyo Rais Dkt. Samia ameitoa leo Aprili 1, 2024 akizungumza waaumini wa Kanisa la WRM kwa njia ya simu ambalo limeadhimisha miaka 17 tangu kuanzishwa kwa huduma yake.

"Mnaposherehekea Pasaka mnajambo la kutafakari, mnapaswa kukaa kwa wema, kukumbuka mafunzo ya Dini zetu, kukaa kwa wema na umoja na kukumbuka matendo ya mitume Wetu," amesema Rais Dkt. Samia na kusisitiza,

"Tutafakari vyema maana ya Pasaka, na tukumbuke ndugu na umoja pale tunapokutanishwa kanisani, niwapongeze kwa maadhimisho hayo,".

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jery Silaa ambaye amemwakilisha Rais Dkt. Samia katika maadhimisho ya miaka 17 tangu kuanzishwa kwa huduma ya Kanisa ya WRM,

Ameahidi kuwa amepokea mambo yote yaliyosemwa katika risala na kwamba atayafikisha kwa Rais Dkt. Samia na yatafanyiwa kazi.

Silaa ametumia fursa hiyo kuwaomba wazazi kuwalea watoto katika njia impasayo Mungu kwani hawataiacha hata watakapokuwa wazee.
 
Kwa upande wake Kiongozi na Mwanzilishi wa Kanisa hilo Prophet Nicolaus Suguye amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa Serikali kulipatia usajili Kanisa hilo.

"Tunashukuru kwa kutupatia rasmi usajili wa Kanisa letu, nasi tunakuombea uzidi kuwa hodari katika kuongoza Taifa letu hili, na uzidi kuwa hodari Duniani," amesema Prophet Suguye.

Prophet Suguye ameahidi kuwa pamoja na kupatiwa usajili huo, amesema kuwa kama Kanisa wapo pamoja na Rais na kwamba watafanya huduma kwa kufuata kanuni, taratibu na Sheria za Nchi, hivyo watakiwa mfano kwa wengine.