Viongozi mbalimbali wa kada ya Elimu wajitokeza katika Hafla ya Kumuaga Afisa Elimu, Mkoa wa Dar es salaam Alhaj Maulid
Na, Vicent Macha DSM.
Wakuu wa shule, Maafisa Elimu pamoja na Wadau wote wa kada ya Elimu wametakiwa kumpa ushirikiano Afisa Elimu mpya wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Gifty Kyando ili kuweza kutimiza maono ya Rais Dkt. Samia katika kukuza na kuendeleza elimu nchini.
Hayo yameelezwa na aliyekuwa Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam ambae sasa ni Mkurugenzi wa Idara ya Elimu msingi, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Bw. Alhaj Maulid katika tafrija maalum ya kumuaga iliyofanyika Mbezi Beach, Dar es salaam.
Katika hafla hiyo iliyoudhuriwa na Wakuu wa shule, Walimu wakuu, Maafisa Elimu kata na Wilaya, Watumishi wa Afisa Elimu Mkoa wa Dar es salaam na wadau mbalimbali wa kada Elimu.
Mkurugenzi Maulid amewaasa walimu na Viongozi mbalimbali waliyopo katika kada hiyo kuwa ni watu wa kupenda kusikiliza kuliko kuongea. "Napenda kuwaasa Walimu wenzangu asilimia 80 muwe mnasikiliza na asilimia 20 pekee ndio muwe mnaongea, mpende kuwakiliza wateja wenu kwani wao ndio sababu ya nyinyi kuwepo hapo mlipo" alisema Maulid
Ameongeza kwa kusema kuwa anawapongeza walimu wote kwa kumuheshimisha kwa kufanya vizuri kitika mitihani mbalimbali na kuufanya mkoa wa Dar es salaam kuendelea kuwa juu kielimu.
Na mwisho amewashukuru kwa ushirikiano wao waliompa kwa kipindi chote alichokuwa katika mkoa huu wa Dar es salaam na kuwaomba waendelee kushirikiana vema na Afisa Elimu mpya Bw. Gifty Kyando ili kuendelea kuilinda heshima iliyopo, lakini pia kuendelea kumuheshimisha Afisa Elimu huyo aliyekuja kuziba nafasi yake.
Kwa upande wake Afisa Elimu wa sasa wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Gifty Kyando ameendelea kuwaomba walimu na watumishi mbalimbali wa mkoa huo kuweza kuwa na umoja na ushirikiano ili kuendeleza mazuri yaliyopo Dar es salaam.
Afisa Elimu huyo ameongeza kwa kusema kuwa wana Dar es salaam wamempa deni.
"Wana Dar es salaam mmenipa deni nami sina budi kulilipa, nitahakikisha nitalilipa kwa maana kwa hiki mlichonipatia itakuwa sehemu ya kumbukumbu kwangu ya kwamba nadaiwa na njia za kulilipa ni kwa kuwaombea pamoja na kufanya kazi kwa bidii" Alisema Kyando
Aidha ameendelea kusisitiza kuwa Dar es salaam ni kipimo cha mikoa yote Tanzania kwa wengine wote wanajipima kwetu kuona wamefanikiwa kwa kiwango gani hivyo tupige kazi ili kuendelea kuheshimisha mkoa huu ambao ndio dira ya mikoa mingine, lakini pia kuheshimisha nchi na kiongozi wetu Dkt. Rais Samia
Kamati ya maandalizi wakipokea zawadi ya keki katika hafla ya Kumuaga rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Dar es salaam Bw. Alhaj Maulid. |
Baadhi ya wanakamati ya maandalizi wakimkabidhi zawadi ya keki Afisa Elimu wa sasa wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Gifty Kyando ishara ya kumkaribisha rasmi Mkoa wa Dar es salaam. |
Hakuna maoni
Chapisha Maoni