Na Mussa Augustine.
Benki ya Akiba (ACB)
imezindua rasmi huduma ya kadi za VISA ambazo ni mahususi kwa kufanya huduma za
miala ya kifedha ambapo inauwezo wa kutumika sehemu yoyote Duniani.
Akizungumza wakati wa
uzinduzi huo wa ACB VISA, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ,Silvest Arumasi
amesema kwamba Benki ya ACB inafanya maboresho makubwa ya huduma za kifedha kwa
wateja wake ili kuendana na mahitaji ya soko.
Aidha amesema kwamba
maboreshao hayo yatasaidia kukidhi matarajio ya wateja ambapo hivi sasa
huduma nyingi za kibenki zinatolewa kidigitali nakusaidia wateja kupata huduma
kwa haraka na rahisi zaidi.
"Huduma za ACB
VISA CARD zinamrahisishia mteja kufanya miamala mbalimbali kidigitali mfano
; kutoa pesa kwenye ATM mbalimbali za VISA popote Duniani, na kufanya manunuzi
mtandaoni, kufanya malipo kwenye vituo vya mafuta, kwenye migahawa na kwenye
maduka makubwa ( Shopping malls & supermarkets) na nyingine nyingi"
amesema Silvest
Bw. Silvest
amewashukuru wateja wote kwa kuendelea kuiamini ACB na kufanya biashara kupitia
benki hiyo, nakuwaomba Wajasiriamali na Wafanyakazi kutoka taasisi za umma na
binafsi kujiunga na benki ya ACB ili kufurahia huduma bora zaidi kwa uharaka,
unafuu na usalama.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni