Na Mussa Augustine.
Mkurugenzi wa Maendeleo Benki Plc’ Dkt. Ibrahim Mwangaraba amesema
kuwa kuwa Benki hiyo imeendelea kukua mwaka hadi mwaka ambapo kwa Mwaka 2023
matokeo ya kifedha yameonesha kukua kwa faida ya asilimia 66% baada ya kodi na
kufanya faida baada ya kodi kuongezeka hadi shilingi Bilioni 2.3 kutoka
shilingi Bilioni 1.4 Mwaka 2022.
Hayo ameyasema leo April 17/2024 wakati akizungumza na
waandishi wa habari Katika ofisi za Benki hiyo jijini Dar es Salaam wakati
akitoa taarifa ya Maendeleo ya Benki hiyo kwa Mwaka 2023 nakusema kuwa Baadhi ya vichocheo vya
mafanikio ya Benki hiyo ni pamoja na ukuaji wa faida baada
Benki hiyo ambayo niya kwanza nchini
kuorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE,) na kuweka historia ya
kuwa benki yenye faida kwa miaka tisa mfululizo tangu mwaka wa pili wa
kuanzishwa kwake ni pamoja na kuimarika kwa ubora wa mikopo kutoka mikopo
chechefu ya asilimia 5.2 mwaka 2022 hadi kufikia asilimia 4.95 mwaka 2023
kulikosababishwa na kuimarika kwa hali uchumi na kufanya wateja wao kulipa
mikopo kwa wakati.
"Ndugu waandishi wa habari ukuaji
huo wa faida wa kuvutia umechangiwa
zaidi na mikakati mizuri ambayo benki ilijiwekea kwa mwaka 2023 pamoja na
usimamizi bora wa watendaji na wafanyakazi wa benki hiyo kwa kushirikiana na
wateja na wadau mbalimbali." Amesema Mwangalaba.
Dkt Mwangaraba ameendlea kusema kuwa mali za benki zimeongezeka kwa asilimia
17% kutoka shilingi za kitanzania Bilioni 107.0 kwa mwaka 2022 hadi kufikia
shilingi Bilioni 125.0 kwa mwaka 2023 huku mtaji wa benki ukiimarika kwa
asilimia 12%kutoka shilingi za kitanzania Bilioni 17 kwa mwaka 2022 hadi
shilingi Bilioni 19 kwa mwaka 2023.
Akizungumzia kuhusiana mtaji na
kuwafikia wananchi katika Mikoa nchini kote Dr. Mwangalaba amesema kuwa, Benki
hiyo imefikisha mtaji wa Shilingi Bilioni 19 ambao unakidhi benki kufanya kazi
nchini kote ili kuhakikisha wateja wake wanapata mikopo na kuendleza biashara
zao bila tatizo lolote.
“Kutokana na kuweza kukuza mtaji na
kufikia bilioni 19 kunaiwezesha benk hii kufanyakazi nchi nzima hivyo
tumeshaanza mazungumzo na Benki Kuu
ya Tanzania (BOT,) ili tupate kibali cha kufungua matawi Mikoani na kuwahudumia
Watanzania wengi zaidi zaidi,na mazungumzo yetu yapo katika hatua nzuri”amesema
Dkt.Mwangaraba
Nakuongeza kuwa “kumekuwa na ongezeko la Amana za wateja kwa
asilimia 15 kutoka shilingi Bilioni 78.0 mwaka 2022 hadi kufikia shilingi
Bilioni 90.0 kwa mwaka 2023.
Amesema kuwa mikopo ya wateja
imeongezeka kwa asilimia 21 kutoka shilingi za kitanzania Bilioni 61.0 hadi
shilingi za kitanzania Bilioni 74.0 kwa mwaka 2023,ukuaji huo utaendelea kwa
kuwa Benki imejipanga kutoa huduma kwa ufanisi zaidi kwa wateja wake.
Aidha Mkurugenzi huyo wa Mandeleo
Bank Plc amefafanua kuwa utendaji kazi bora wa mwaka 2023 umejenga msingi
thabiti wa utendaji kwa mwaka 2024 ambapo wamejipanga kutanua huduma zaidi kwa
kufungua angalau tawi moja na kuongeza mawakala wapya zaidi ya 500 kutokana na
mafanikio makubwa ya mwaka 2023 ambapo walifunga na nakuongeza mawakala 1600
katika mikoa 11 nakufanikiwa kukusanya zaidi
ya Bilioni 5 kila mwezi kama amana kila mwezi kupitia wateja wake.
“Benki inawekeza sana katika
teknolojia na kwa mwaka 2024 tumejipanga kuanzisha huduma mpya za kidigitali
ikiwemo Benki mtandao yaani Internet Banking, mfumo wa ukusanyaji malipo
ikiwemo ada za shule (PCS,) na mikopo kwa njia ya simu ambayo itawezesha benki
kuongeza faida kwa fedha za wanahisa kwa mwaka 2024 na kuboresha njia mbadala
za upatikanaji wa huduma za wateja.
Nakuongeza kuwa "kwa kuonesha
juhudi za kuboresha na kusogeza huduma kwa wateja mwaka huu 2024 tumefungua
tawi jipya Mbagala hapa jijini Dar es Salaam likiwa tawi la tano huku tukiwa na
lengo la kusogeza huduma zetu kwa wakazi wa Mbagala na maeneo jirani.” Amesisitiza
Dkt Mwangaraba.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni