TIRDO YAKABIDHI MASHINE YA KUONDOA GANDA LAINI LA KOROSHO KWA CAMARTEC.
Na Mussa Augustine.
Shirika la
Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda Nchini(TIRDO) limekabidhi Mashine ya Kuondoa
ganda laini la Korosho kwa Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia
vijijini(CAMARTEC) ili kuweza kutoa mafunzo kwa wajasiliamari katika kiwanda
Darasa kilichopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida.
Akizungumza
wakati wa hafla ya Makabidhianao hayo
yaliyofanyika tarehe 29,2024 Makao Makuu ya TIRDO Jijini Dar es salaam ,Mkurugenzi
Mkuu wa TIRDO, Prof.Mkumbukwa Madundo Mtambo amesema kuwa mashine hiyo
imetengenezwa kwa ushirikiano na Shirika la Viwanda Vidogo Nchini (SIDO) pamoja
na TEMDO ikiwa ni utekelezaji wa ombi la CAMARTEC.
Prof.Mtambo
amesema kwamba mashine hiyo itasaidia kutoa mafunzo kwa wajasiliamari
wanaojifunza namna ya kubangua korosho Wilayani Manyoni Mkoani Singida
ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa adhma ya serikali kuhakikisha korosho
zinaongezwa thamani.
“Leo
tunakabidhiana Mashine hii ya kuondoa ganda laini la korosho kwa wenzetu
CAMARTEC ili waweze kutoa mafunzo kwa wajasiliamari waliopo katika kiwanda
darasa cha kubangua korosho Wilayani Manyoni Mkoani Singida”amesema Prof
Mtambo
Nakuongeza
kuwa”Naomba nitumie fursa hii kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuzipatia fedha taasisi mbalimbali kwa ajili ya kuzisaidia taasisi hizo kujiendesha na kutatua
changamoto zinazojitokeza ili kufikia malengo yake.
Kwa upande
wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu CAMARTEC ,Pythias Mtella amesema kwamba Ubanguaji wa
korosho katika kiwanda Darasa umeanza mwezi Machi,nakwamba kwa sasa
wanakabiliwa na chanagamo ya ukosefu wa mashine ya kuondoa ganda laini la
korosho hivyo kupatikana kwa mashine hiyo itasaidia kufanya kazi yao kwa
ufanisi.
Aidha amesema kuwa pamoja na kupatikana kwa Mashine ya Uondoaji wa ganda laini la Korosho bado kuna changamoto iliyobaki ya kupata mashine ya kupaki korosho kwa ajili ya kwenda sokoni.
“Lengo la
serikali ifikapo mwaka 2025/26 asilimia 60 ya korosho ibanguliwe hapa nchini ,nakwamba ifikapo 2030 korosho zote ziweze kubanguliwa hapa nchini,hivyo kwa
sasa inahitajika mafunzo ya kuzalisha wajasiliamari wengi wenye ujuzi wa kuongeza mnyroro
wa thamani kwa zao hilo ili kufikia malengo hayo.
Nae Mhandisi
Idara ya Maendeleo kutoka TIRDO, Mh.Atupele Kilindu amesema kwamba mashine hiyo ya
kuondoa ganda laini la korosho inauwezo wa kuondoa ganda kwa kilo 350 kwa saa nakwamba
imegharimu kiasi cha shilingi milio 40 kukamilika kwake.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni