Zinazobamba

MIAKA 10 YA E.FM YAJA NA JUKWAA LA"KITAA HUBS"KWA AJILI YA VIJANA KUPATA AJIRA.


Na Mussa Augustine 

Katika kutimiza miaka 10 tangua kuanzishwa kwa  kituo cha redio E.FM,kituo hicho kimeanzisha Jukwaa lijulikanalo kama “ Kitaa Hub”likilenga kusaidia vijana kupata ajira na kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza leo Aprili 15,2024 Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Francis Sizza maarufu kama Majizzo amesema kupitia kituo cha EFM atatimiza maono yake ya kuwainua vijana kiuchumi kupitia kampeni ya Majizzo Jobs Campaign.

Majizzo amesema jukwaa la Kitaa Hubs litakuwa jukwaa mahususi lenye lengo la kuwapa vijana nafasi ya kujifunza, kukua na hata kushindana katika soko la ndani na kimataifa.

“ Lengo letu  ni kufikia kundi kubwa la vijana kwenye field tofauti tofauti, naongelea vinyozi, fundi uashi, wapishi, wasusi, dada wa kazi, madereva, wasanii, waandishi wa nyimbo, DJS na graduates na wengine wengi Kwa kifupi ni uwanja wa kujidai onyesha uwezo wako” Amesema Majjizo.

 Kwa upande wake mjumbe wa timu inayosimamia jukwaa hilo Dkt Albert Komba amesema kwamba jukwaa la Kitaa hubs litasaidia kuwajengea uwezo vijana wanaotafuta ajira na kuwaunganisha na waajiri Kwa urahisi zaidi.

Aidha amesema kwa sasa kiwango Cha ajira chini kipo chini hivyo serikali na taasisi binafsi hazina budi kushirikiana kutafuta mwarobaini wa tatizo Hilo nakisusisitiza kuwa kupitia Kitaa hubs intasiadia kupunguza tatizo la ajira Kwa vijana ambao Wana vipaji vya aina mbalimbali.

 “Hili jukwaa la Kitaa hubs pamoja na Majizzo jobs Compaign itaweza kukutanisha vijana nchi nzima ili kuweza kuonyesha vipaji vyao,naamini kuanzishwa kwa jukwaa hili itasaidia vijana kutoa mawazo yao,bunifu zao na kuweza kufikia ndoto zao Kwa urahisi zaidi” amesema Dkt Komba.

 Hata hivyo   vijana waliojitokeza  katika mkutano huo  wamepongeza jitihada za kuanzishwa kwa jukwaa la Kitaa hubs kwani litawasaidia kuwasimamia  kupata kazi nzuri na zenye staha huku wakisisitiza kuwepo kwa ulinzi wa usalama wa taarifa zao kwenye  tovuti ya kuhifadhi taarifa hizo.

Hakuna maoni