TANZANIA NA HUNGARY ZASAINI MKATABA WA KUSHIRIKIANA SEKTA YA MAJI NA USAFIRI WA ANGA
NA
Mussa Augustine.
Tanzania na Hungary zimetiliana saini Mikataba ya kushirikiana katika Masuala ya Maji na Usafiri wa Anga nakwamba Hungary iko Mbioni kufungua ubalozi wake hapa nchini.
Akizungumza leo Machi 24,2024 jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Mh. Januari Makamba amesema kuwa hatua hiyo inatokana na Rais wa Hungary kuja Nchini Tanzania Mwaka 2023,nakusababisha muendelezo wa ushirikiano wa muda mrefu uliopo baina ya Nchizo.
"Tumepata ugeni kutoka Hungary na hii inakuja baada ya Rais wao kuja hapa Tanzania mwaka jana na kusababisha kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu uliopo baina ya nchini zetu mbili," amesema Mh.Makamba .
Aidha ameongeza kuwa Mazungumzo hayo baina yake na ujumbe kutoka Hungary ulioongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa taifa hilo, Peter Szijjà rtò wamekubaliana mambo kushirikiana mambo mbalimbali ikiwemo kuanzisha safari za anga ya moja kwa moja hadi hapa nchini.
Waziri Makamba amefafanua kuwa safari za anga ya moja kwa moja kutoka Hungary kuja Tanzania itasaidia kutanua wigo wa kibiashara baina ya mataifa hayo mawili.
“Hatua hii pia itaongeza watalii wanaotoka Hungary kuja Tanzania ambapo kwa miaka miwili iliyopita watalii 5000 waliingia hapa nchini kutoka katika nchi hiyo na mwaka jana waliongezeka na kufikia 11,000,sasa tutakua katika hatua nzuri zaidi” Amesisitiza Waziri Makamba
Aidha amesema kuwa ongezeko hilo la watalii wanaotoka Hungary kuja Tanzania litaongezeka pindi itakapoanzishwa safari ya anga ya Moja kwa Moja hali ambayo itasaidia kufungua fursa nyingi za kibiashara.
Aidha katika sekta ya kibiashara Nchi hizo zimekubaliana kwa pamoja kuandaa amakongamano ya sekta binafsi yatakayofanyika Hungary na Tanzania.
Pia wamekubaliana kuendeleza ushiriano kwenye elimu na kuongeza scholarship kwa Watanzania kwenda kusoma Hungary na Tanzania itakuwa ikitoa nafasi tano kwa vijana wa nchi hiyo kuja kusoma hapa nchini katika vyuo mbalimbali vilivyopo kila mwaka.
"Hadi sasa tayari wanafunzi 146 wa kitanzania wamepata fursa ya kusoma nchini Hungary na kila mwaka tunapeleka vijana wetu kusoma huko na hiyo imekuja baada ya wenzetu mwaka 2018 kuanzisha programu ya Scholarship amesema.
Amesema kuwa sababu ya kuchukua hatua ya Kusaini mkataba wa kushirikiana katika Sekta ya Maji ni kutokana na taifa hilo kuwa kuongoza katika teknolojia ya kudhibiti mafuliko, maji taka na ya kutumia.
“Maarifa yao Makubwa katika sekta ya maji ndio imetuvutia kusaini mkataba unaohusu masuala hayo ili nasi tupate utaalamu wa kutosha katika nyanja hiyo, amesema Waziri Makamba mbele ya Waandishi wa habari
Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Hungary, Peter Szijjà rtò amesema kusaini Mkataba wa usafri wa anga utasaidia kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya mataifa hayo mawili,nakwamba mikataba hiyo itatekelezwa kama walivyokubaliana.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni