Sheikh Othman Michaela: hatutafunga huduma zetu, wananchi watoe hofu
Mtalaamu wa kueneza
da’aawa kwa umma kupitia kitabu kitukufu cha Quran na suna za Bw. Mtume
Muhammad (saw) Sheikh Othmani Michael amewatoa hofu waislamu na wasio kuwa
waislamu kuwa huduma zake zitaendelea kupatikana kama kawaida na kwamba
kilichotokea ni sehehmu katika changamoto za kazi.
Alisema anaamini
kazi anyoifanya ni muhimu, hivyo ataendelea nayo kama kawaida kwani huo ni wito ambao analazimika kuufanyia kazi ili
watu wapate kunufaika.
Akizungumza katika
mahojiano maalum na mtandao wa fullhabari blog, ofisini kwake Sheikh alisema
mpaka ofisi yake imepokea kazi nyingi kutoka kwa wananchi ambao wanahitaji
huduma, hivyo hawana mpango wa kufunga huduma zao.
Sheikh Othman
ambaye pia ni tabibu wa da’aawa za kisunna ameongeza kusema kuwa kupitia ofisi
yake waislamu na wasio waislamu waliweza kutatuliwa changamoto zao na faida
nyingi imepatikana ikiwamo watu wengine kuiga anachokifanya.
![]() |
“Kupitia mitandao
ninayoiongoza watu wengi wamepata kufaidika, mpaka sasa nchi zingine zimeiga
utaratibu niofanya, kuna watu wameanzisha maudhi ya papo kwa papo (live
progammes), wengine wanafanya ya kurekodi (recording), hivyo tutaendelea na
kazi hiyo,” alisema.
Mimi tamaa yangu ni
kuona nasuluhisha matatizo mengi kwa kadri ya uwezo wangu, natamani siku moja
nikikutana na Allah niwe nimesuluhisha kesi bilioni moja, na nikiulizwa niwe na
cha kujibu
Hivi karibuni
Baraza kuu la waislamu mkoa wa Dar es salaam limemuita na kufanya mazungumzo na
Sheikh Othmani kwa lengo la kujua sababu za kusambaza video ambayo imeleta
sintofahamu.
Sheikh alisambaza
video katika mitandao ya kijamii akifanya mahojiano na wanawake wawili, binti
na mama mzazi waliokwenda ofisini kwake kupata suluhu ya changamoto
waliyoipata.
Katika kikao hicho
Baraza la masheikh wa mkoa limebaini kuwa kilichokuwa kinasambaa mitandaoni
hakikuwa na ukweli wowote bali ni igizo la kisa cha kweli kilichotokea huko
nyuma.
Sheikh Alhad Musa
Salum alitumia cheo chake kuwaomba waislamu kokote nchini kumdhania kheri
Sheikh Othmani Michael kwani baraza lake limebaini kuwa hakuwa na nia mbaya
katika kutengeneza video hiyo.
Sheikh Othmani
aliwahi kusuluhisha kisa kama hicho, kutokana na uzito wa kisa chenyewe, busara
ilimuongoza kucheza kisa hicho kwa lengo la kufikisha daawa kwa umma, bahati
mbaya watu wameipokea tofauti.
Aidha alibainisha
kuwa Bakwata haiwakatazi Masheikh,
maimam, maostazi kushughulikia migogoro ya waislamu sababu baraza lenyewe
linaanzia huko ngazi ya jamii.
Aidha Sheikh Alhadi
alimsifu Sheikh Othman Michael kwa kazi kubwa anayoifanya ya daawa na
kusisitiza kuwa wao kama walezi wanamuunga mkono kwa kazi hiyo ya kuitengeneza
jamii, amewaomba waislamu kumchukulia udhuru kwa tukio hili kwani nia yake
ilikuwa ni njema ya kufikisha ujumbe.
Aidha amekosoa
tabia ya waislamu kukosoana kupitia vyombo vya habari huku akishauri njia nzuri
ya kukosoa ni kutafutana na kujua ukweli kisa kuchukua hatua stahiki.


No comments
Post a Comment