Ukeketaji bado ni tatizo kubwa Tanzania, wadau washauliwa kuvunja ukimya
Na mwandishi wetu
Mkurugenzi wa Jukwaa la utu wa mtoto (CDF) Koshuma Mtengeti
amewashauri viongozi wa dini, serikali na wadau wengine hapa nchini kukemea
vitendo vya ukeketaji kwani tatizo hilo bado lipo na linachangia katika
unyanyasaji wa kijinsia
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mtaalamu huyo wa
masuala ya utetezi wa mtoto, amekili kuwa licha ya jitihada ambazo
zinachukuliwa kunahitajika nguvu ya pamoja ili kuodnoa tatizo hilo.
Alisema Pamoja na jitihada ambazo serikali imekuwa ikizichukua bado
kuna baadhi ya mikoa waifanya kazi ya ukeketaji kama sehehmu ya kuleta kipato
lakini pia wanasiasa wamekuwa wakichangia kurejesha nyuma nguvu ya kupambana na
wakeketaji.
“Unajua kwa baadhi ya makabila hili suala wamelifanya ni sehehmu
ya kujipatia kipato, lakini pia kuna wanasiasa ambao wanasema hadharani kuwa
hawa ni wapiga kura wangu waacheni watekeleze mila, sasa hapo bado kuna shida,”
alisema.
Aidha Koshuma ameshauri serikali kuwekeza elimu katika kuwawezesha wananchi kiuchumi hasa maeneno ambayo yanaongoza katika zoezi la ukeketaji, dhamira ikiwa ni kuwavutia watu waachane na ukeketaji na wafanye kazi halali.
Koshuma ambaye ameyazungumza hayo wakati alipotakiwa kutoa
tathmini yake juu ya ukeketaji Tanzania,
Tukiwa tunaelekea siku ya kupinga vitendo vya ukeketaji duniani lazima tujitakali, tumefanikiwa kiasi gani,
ukweli tumefanikiwa lakini bado tunayo kazi ya kufanya.
Alisema takwimu za shirika la afya duniani zinaonyesha kuwa
vitendo hivyo vimepungua kutoka asilimia 18 mwaka 1996 hadi asilimia 10 mwaka
2016
Alisema mafanikio hayo yamepatikana kutokana na ushirikiano na
jitihada kati ya serikali na Asasi za kiraia pamoja na wadau wengine wa
serikali kupinga ukeketaji na kujikita zaidi katika kutoa elimu ya kubadili
mitizamo ya jamii juu ya mtoto wa kike.
Amezitaja baadhi ya sababu ambazo zimekuwa zikitajwa kuendelea
kwa vitendo ivyo ni pamoja na njia ya kuonyesha kuwa msichana amekuwa mwanamke
kamili na tayali kuweza kubeba majukumu ya kifamilia pamoja na kujiongezea kipato
kwa wanaofanya kazi hiyo (angariba).
Mikoa ambayo imekithiri kwa vitendo vya ukeketaji ni pamoja na Manyara
ambayo inaongoza kwa kuwa na asilimia 58, Dodoma asilimia 47, Arusha asilimia
41 na Mara asilimia 32.

No comments
Post a Comment