NEEC, GGML kukutana na wajasiliamali na watoa huduma 150 mkoani Geita
Issack Tadheo, Dar
es salaam
Baraza la uwezeshaji
wananchi kiuchumi kwa kushirikiana na Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) wameandaa
mafunzo kwa vitendo kwa kwa
wajasiliamali na watoa huduma 150 ambayo atafanyika katika ofisi ya sido mkoani
Geita.
Mafunzo kwa
wajasiliamali na watoa huduma
yanatarajiwa kuanza machi, 8 2021 na kukamilika kwake mach 19, 2021 na
yatahusisha stadi mbalimbali ikiwamo usindikaji wa vyakula, utengenezaji wa
sabuni, chaki, mabegi, na urembo wa wanawake.
Akizungumza na
Fullhabari Blog, katibu mtendaji wa Baraza la taifa la uwezeshaji wananchi
kiuchui, Bibi Beng’I Issa amesema hiyo ni fursa kwa wakazi na wafanya biashara
wa mkoa wa geita kujitokeza katika mafunzo hayo kwani ni muhimu sana kwa kazi
zao.
Lengo la mafunzo ni
kuwawezesha washiriki kuboresha bidhaa zao ili zikizi viwango vya soko pamoja na kupata alama za ubora kutoka
mamlaka ya viwango Tanzania pamoja na
kupata alama za utambuzi wa bidhaa zao kutoka GSI
Pogram hii
itatekelezwa kwa kipindi cha Mwaka mmoja nakunufaisha wajasilliamali zaidi ya
300 (Miatatu), ikiwemo mpaka sasa pogramu hii imewezesha mafunzo ya usimaminzi
wa biashara na ushindani katika zabuni kwa wajaliamali wapatao 365 katika
mafunzo ya awamu ya kwanza,
Pia katika mafunzo ya awamu ya pili watoa
huduma 148 (Miamoja arubaini nanane) watapatiwa Elimu na Mbinu za Kujiunga Katika
Kongamano
Ili kuwaongezea
ujuzi na nguvu za kushindana vema ktk soko la pamoja, Aidha katika kutekeleza
pogramu hii baraza kwa kushirikiana na Mgodi wa Dhahabu wa Geita wameandaa
mafunzo kwa vitendo kwa wajaslliamali na watoa Huduma 150 (Miamoja hamsin)
ambayo yatafanyika mkoan geita Ambayo yatahusisha Stadi mbalimbali kama vile
usindikaji wa vyakula utengenezaji wa sabuni na batiki,ushonaji, kudarizi,
utengenezaji chaki, mifuko mbadala, mabegi na urembo wa wanawake, ufugagi kuku
na kilimo cha bustani, lengo la mafunzo haya nikuwawezesha kutengeneza
nakuboresha bidhaa zao ili zikidhi viwango vya soko la pamoja ili ziweze
kutambuliwa na mamlaka ya viwango nchini (TBS)

No comments
Post a Comment