Zinazobamba

GUARDIANS OF THE PEAK SEASON 2 WANAFUNZI WATANO WAPATA FURSA YA KUTEMBELEA MLIMA KILIMANJARO .

Lengo ni kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi na uhifadhi wa Mazingira kuzunguka Mlima huo.

Na Musaa Augustine

Msimu wa pili wa Guardians Of The Peak umefanikiwa kupata wanafunzi watano  kati ya 42 kutoka Vyuo Vikuu hapa nchini ambao watakuwa mabalozi wa kuhamasisha Nishati Safi ya Kupikia katika maeneo yanayozunguka Mlima Kilimanjaro

Wanafunzi hao watano ambao wamepatikana baada ya mchujo watajumuika na wadau wengine kupanda Mlima Kilimanjaro kuanzia Januari 20 hadi 31 mwaka huu lengo mahususi nai kuutangaza kimataifa na kuhamasisha uhifadhi wa mazingira kwa jamii zinazouzunguka mlima huo.

Akizungumza katika halfla ya utangazaja wa jambo hilo, Januari 14, 2026 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Filamu,Emmanuel Ndumukwa,  kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Dkt. Gervas Kasiga, amesema shughul hiyo itatilia mkazo umuhimu wa nishati safi ya kupikia

Pia nashukuru kuona wanafunzi wa vyuo nao kujumuishwa katika jambo hili muhimu kwa mustakabali ya nchi yetu naamini watakuwa mabalozi wazuri katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi katika mlima Kilimanjaro ikizingatiwa kuwa kuna miti mingi ya asili ambayo inazunguka mlima na inahitaji kulindwa.

Amesema kuwa katika msimu huu wa pili uzalishaji wa tamthilia ya (documentary series) Guardians of the Peak yamekamilika na jamii itajionea filamu itakayosimulia chagamoto kadhaa za uhifadhi wa mazingira katika mlima na namna ya kuzitatua ili kufikia malengo.

Ameongeza kuwa msimu wa pili unatarajiwa kuingia kwa undani zaidi katika uhalisia unaoukabili mlima mrefu zaidi barani Afrika, kwa kuangazia juhudi za uhifadhi, ushiriki wa jamii zinazouzunguka mlima huo, pamoja na mizani nyeti kati ya uhifadhi wa mazingira na shughuli za utalii.

mebainisha kuwa kupitia mchakato huo sauti ya Tanzania itapenya katika majukwaa ya kimataifa yanayohusu mazingira na filamu za maandishi, pamoja na kuimarisha taswira ya nchi kimataifa.

 Amesisitiza kwamba Serikali itaendelea kuwezesha na kuunga mkono miradi inayotumia filamu kama chombo cha elimu, mabadiliko ya kijamii na kuitangaza Tanzania kimataifa.

Aidha, aliwahimiza watayarishaji wa filamu, wasanii wa maonesho, taasisi za serikali, sekta binafsi pamoja na vyombo vya habari kushirikiana na kuunga mkono Guardians of the Peak na kazi nyingine zinazochanganya ubunifu wa kisanaa na maslahi ya taifa na dunia kwa ujumla.

No comments