Zinazobamba

WANANCHI KATA YA BUYUNI WASIFIA ZOEZI LA UTOAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA.

*Wananchi zaidi ya 200 wajitokeza kupata vitambulisho vya Taifa.
*Wampongeza Diwani wao na Serikali kwa ujumla kuwasogezea karibu huduma hiyo.

Na Mussa Augustine.

Diwani wa kata ya Buyuni Jijini Dar es salaam Jesca Msolla(CCM) amewahimiza Wananchi wa kata hiyo kujitokeza kwa wingi kupata kitambulisho cha Taifa (NIDA)ili waweze kupata fursa mbalimbali ikiwemo mikopo kutoka Taasisi za kifedha.

Diwani huyo amesema hayo leo Januari 19,2026 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari kando ya uzinduzi wa zoezi la utoaji wa vitambulisho hivyo linaloendelea kufanyika katika Ofisi za Mtendaji wa kata ya Buyuni Jimbo la Ukonga.

Aidha amesema kuwa hatua ya utoaji wa Vitambulisho hivyo imetokana na kupata maombi  mbalimbali kutoka kwa Wananchi ambao wamekua wakikosa fursa za kupata mikopo kutoka taasisi za kifedha hali ambayo inawafanya washindwe kujikwamua kiuchumi.

"Tumeamua kufanya zoezi hili kwa ajili ya kuwasaidia Wananchi wapate vitambulisho vya NIDA kwasababu wengi wao walikua wananifuata Ofisini nakuniomba niwasadie, kwahiyo Mamlaka zote zipo hapa ikiwemo NIDA,Wanasheria, pamoja na Uhamiaji ili tutoe hivi vitambulisho kwa Wananchi"amesema Diwani Msolla. 

Kwanza kabisa namshukuru Mwenyezi Mungu leo tarehe 19 kama tulivyokua tumeadhimia kuwepo na uzinduzi wa mamlaka ya NIDA kuja kufanya huduma katika kata yangu ya Buyuni,mimi nipo hapa kama mwakilishi wa Wananchi wote wa kata ya Buyuni. "Amesema 

Nakuongeza kuwa "niliona katika kila fursa ambazo mwananchi wa kata ya Buyuni anataka kwenda kupata anaulizwa kitambulisho cha NIDA,nikaona ni vyema kwenda kutafuta hii fursa namshukuru Mwenyezi Mungu kupitia mamlaka ya NIDA niliweza kukubaliwa". 

Aidha amesema kuwa kumekuwepo na changamoto ya baadhi ya Wananchi kwenda na nyaraka ambazo hazijakamilika hivyo Elimu inaendelea kutolewa kwa Wananchi kwa ajili ya kuondokana na changamoto hiyo. 

"Leo hapa tumekua na changamoto kutokana na watu kutokujua nini stahiki wanakuja kufanya,kuna wale waliopoteza vitambulisho vyao sio hapa ni kwenda kule kwenye Ofisi kubwa ambako ni Mombasa kwa kanda hii ya Ilala,lakini hapa tulikua tunaanza kwa wale ambao hawana kabisa NIDA."amesema 

Aidha Diwani Msolla amesema kuwa Wananchi wa Kata ya Buyuni wengi wao ni Wajasilimari wenye kiwango cha chini Cha shilingi milioni 4,huku biashara zao ni kilimo pamoja na kutembeza vitu vidogovidogo.

"Wananchi wangu ni wapenda maendeleo,na kutokana na fursa ya mikopo ya asilimia 10 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan zinahitajika Taasisi za fedha,ambapo ni lazima uwe na kitambulisho cha NIDA  ndipo ndipo upate mikopo,nilipowaeleimisha Wananchi nakuwambia NIDA nikipaumbele wamenielewa ndio maana wamejitokeza kwa wingi." Amesema.
Naye balozi wa zoezi hilo Heri Shaban amesema kwamba zoezi la utoaji wa vitambulisho vya Taifa lilianza katika Jimbo la Segerea Januari 5 hadi 16 nakwamba leo Januari 19,2926 limezinduliwa Jimbo la Ukonga katika kata ya Buyuni na Chanika,na linatarajiwa kufikia tamati Januari 30 mwaka huu.

"Tunaomba Wananchi wote ndani ya Jimbo la Ukonga kata ya Buyuni na Chanika,Zingiziwa na kata zilizopo jirani waje kupata huduma huduma hii kwani dhumuni ni kuhakikisha  Wananchi wote wanatambulika nakupata vitambulisho vya Taifa."amesema balozi huyo.

Hata hivyo baadhi ya Wananchi waliojitokeza kuchukua vitambulisho hivyo akiwemo Mbaraka Hamis Kitonge,Sapta Abeid Tamba pamoja na Mwidini Adam wamempongeza Diwani wa Kata hiyo ya Buyuni pamoja na Serikali kwa ujumla kuleta karibu zoezi la vitambulisho vya Taifa katika kata hiyo.



No comments