Waziri wa nishati ataka wawekezaji kuzalisha vifaa vya kusafirisha gesi hapa nchini
Mwandishi wetu, Dar es salaam.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard
Kalemani ametoa wito kwa wadau wa viwanda kutengeneza Vifaa vya kusafirisha
nishati ya mafuta na gesi hapa nchini dhamira ikiwa ni kuharakisha mchako wa kuanza
miradi ya usambazaji lakini pia kupunguza gharama za uzalshaji.
Alisema uhitaji wa mabomba kwa miradi
inayoendelea bado ni mkubwa na kwamba hadi sasa mahitaji ya mabomba ya gesi ni
kilometa zisizopungua 2,250 na mita za luku ni 8,000 hadi 10,000 kwa
mwaka .
Aidha akizungumzia kasi ya
usambazaji wa mabomba ya gesi majumbani, Kalemani alisema kuna mafanikio
makubwa yamepatikana ikiwamo usambazaji huo kuongezeka kutoka Kaya 70 hadi
kufikia Kaya 1000 kwa Miaka mitatu.
Aliongeza kusema kuwa kuagiza vifaa
nje ya nchi kunapoteza mapato ya nchi, agizo alilolitoa linalenga kulinda
mapato, uzalishaji wa mabomba koki ,vyuma, nyaya utasaidia kujenga uchumi
wa nchi kupitia sekta ya viwanda ,"Dkt.Kalemani .
Faida ya kuzalisha mabomba nchini
itasaidia kuongezeka kwa kasi ya kusambaza gesi na hivyo kuwapa nishati
wananchi kwa wakati.
Naye Naibu Waziri wa Wizara
hiyo Stephen Byabato amesema serikali inaendelea kutekeleza ilani
ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuendelea kuwaunganisha nishati ya umeme
mjini na vijijini.
Alisema Rais Dkt.Magufuli anaamini
vijana wana uwezo kiutendaji ndio maana amemteua kumsaidia kutekeleza majukumu
ya Wizara hiyo chini ya Waziri Dkt.Kalemani.
Awali akizungumza kwenye Mkutano
huo, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Maendeleo la Petroli TPDC Dkt. James
Mataragio amesema wanaendelea na ujenzi wa vituo vitano vya kujaza gesi asilia
kwenye magari katika mkoa wa dar es salaam huku kukiwa na mpango wa kupeleka
nishati hiyo jijini Dodoma.


No comments
Post a Comment