JUVENTUS KUPEWA PIRLO KUTAACHA KUMBUKUMBU NZITO NCHINI ITALIA
Siku ya tarehe 9 mwezi wa 10 mwaka 2017 vyombo vya habari
mbalimbali vya kiulimwengu vilitangaza habari ya kustaafu kwa soka kwa gwiji la
soka la italia Andrea Pirlo. pirlo ametangaza rasmi kwamba mwishoni mwa mwaka
huu ataachana rasmi na mchezo wa soka kwani umri umeshamtupa mkono kwani ana
umri wa miaka 38 na pia amekuwa anapata majeraha mara kwa mara na hana uwezo wa
kuendelea tena na soka la ushindani.
Pirlo ambaye katika maisha yake ya soka amecheza jumla ya
michezo 948 na amefunga jumla ya magoli 111 na kubeba jumla ya makombe 19. Conte
ambaye mwanzoni mwa mwaka 2018 alikuwa gumzo kwenye vyombo vya habari vya
nchini italia baada ya kutamka wazi kwamba katika soka la italia kwa sasa hakuna
anayecheza kama yeye. hili lilizua mjadala na ilitokana baada ya waandishi wa
habari kudai kwamba kiungo wa timu ya PSG ya Ufaransa Marco Verratti kwamba
ndiye mrithi wa Pirlo. Veratti bado hajaweza kumfikia Pirlo kikweli kwani hata
theluthi ya mafanikio ya Pirlo hajayafikia.Pirlo aliweza kumfanya Ronaldo de
Lima aonekane ni hatari zaidi wakati wanacheza pamoja katika kikosi cha Inter
Milan. Aliweza kumlea vizuri Pogba na kumfanya kuwa ni mchezaji wa kiwango cha
dunia wakati walipokuwa wanacheza pamoja katika kikosi cha Juventus.
Binafsi nitamkumbuka Pirlo kwa soka safi alilolionyesha
wakati anachezea klabu ya AC MILAN mnamo mwanzoni mwa miaka ya 2000.
alitengeneza ushirikiano mzuri sanana straika wa kiyukraini Andriy Schevchenko
ambapo kwa pamoja walishinda makombe kadhaa ikiwemo ligi ya Italia na kombe la
klabu bingwa ulaya. alimfanya Schevchenko awe gumzo kubwa sana barani ulaya
kutokana na kumpatia assisti za kutosha za kumfanya afunge mabao mengi sana.
waitaliano wanamkumbuka kwa kiwango chake maridadi alichokionyesha kwenye kombe
la dunia mwaka 2006 ambapo aliisaidia timu yake kushinda kombe hilo.
Wachambuzi wengi wa soka waliona mda mrefu njia ya
baadaye ya Pirlo ni kumfuata aliyekuwa kocha wake wakati wapo Juventus Antonio
Conte katika klabu ya Chelsea kwani amewahi kuonekana mara kadhaa katika uwanja
wa mazoezi wa timu hiyo uliopo Cobham. Cha ajabu mpaka Conte anaondoka katika
jiji la London Pirlo hakupewa kibarua chochote kile katika timu hiyo. Klabu
yake ya AC MILAN nayo halikdhalika ilionekana kama angeweza kupewa kuifundisha
lakini wababe hao maarufu kama “rossoneri” hawakumchukua kama kocha wao na
waliamua kuchukua makocha wengineo. Kilabu chake cha zamani cha INTER MILAN nao
halikadhalika hawakumpatia kibarua na bahati yake ikaangukia kwa kilabu chake
cha zamani cha Juventus baada ya kuamua kuachana na aliyekuwa kocha wao
Maurizio Sarri.
Wayne Rooney katika
mahojiano yake ya hivi karibu aliwahi kusema kwamba katika mechi ya klabu
bingwa ulaya mwaka 2007 dhidi ya AC MILAN aliyekuwa kocha wa wakati huo wa
manchester United Sir alex Ferguson aliwahi kuwapa kazi nzito ya kumdhibiti
pirlo na aliwaambia kwamba aliyekuwa kiungo wa timu hiyo mkorea Park Ji Sung
aliambiwa kwamba ndani ya mechi hiyo jukumu lake ni kuhakikisha mpira haumfikii
Pirlo na hata ukimfikia basi anatakiwa ajitahidi ampokonye na kuhakikisha
kwamba Pirlo hapigi pasi yoyote kwani pasi za Pirlo ni pasi zenye madhara na
wala siyo wa kudhauliwa. Licha ya mipango yote hiyo ya Ferguson katika mechi
hiyo Pirlo alipiga pasi 110 na Manchester United Ilifungwa.
Hayo ni machache katika
kumbukumbu chache zake wakati anacheza mpira leo hii Pirlo ni kocha wa timu ya
Juventus na wiki iliyopita kikosi chake kiliichakaza kikosi cha Barcelona
ambacho kina wachezaji mahiri kama Lionel Messi, Gerald Pique na wengineo
wengi. Kipigo hicho kwa timu ya Barcelona kwa maoni yangu ni salamu kwa vilabu
vikubwa ulaya kwamba kuanzia sasa waiangalie Juventus ya Pirlo kwa jicho
lingine. Sasa natumai ataanza kutuonyesha ujuzi wake katika nyanja hhi mpya.
Natumai Juventus chini ya Pirlo ipo siku itabeba klabu bingwa ulaya sidhani
kama itakwama kama yeye alivyokuwa anakwamba wakati akiwa anaichezea kikosi cha
Juventus. Natumai ataipa mafanikio kama yale aliyoyapata wakati akiwa mchezaji
katika kikosi cha AC MILAN.

No comments
Post a Comment