Ligi ya watoto yaja...Shule zashauriwa kuchukua fomu
Shirikisho
la shule za michezo Tanzania(TASCA) lina mpango wa kuasisi ligi za watoto
ambazo zitachezwa kwa ngazi mbalimbali kuanzia ngazi za wilaya kisha mkoa na
kisha kanda.
Ligi
hizo zitakuwa za makundi mbalimbali kuanzia kundi la chini ya miaka 15, chini
ya miaka 18, na kisha chini ya miaka 21. Ligi hizo zitaratibiwa na TASCA kwa
kupitia wawakilishi wake katika kanda tofauti.
Hayo yamesemwa kupitia ujumbe ambao
ulisambazwa kwa vyombo vya habari vya mitandaoni
Shirikisho
hilo ambalo linatimiza mwaka mmoja toka lisajiliwe limezitaka Shule ambazo zina
mpango wa kushiriki katika ligi hiyo ziwasiliane na wawakilishi wa kanda wa
TASCA au ziwasiliane na kamati kuu kwa ajili ya kupewa formu ya ushiriki na
gharama ya formu hizo ni kiasi cha shilingi za kitanzania elfu hamsini.
Wawakilishi
wa TASCA wanatakiwa wawe makini kuhakikisha kwamba shule zitazoshiriki katika
kanda husika zinaleta wachezaji ambao watakuwa wana umri husika.
wachezaji
ambao watakaowakilisha timu katika mashindano hayo watatakiwa kuwasilisha
nakala za vivuli(photopy) za vyeti vyao vya kuzaliwa. Vyeti hivyo
vitawasilishwa kwa waratibu wa mikoa na kisha vitawasilishwa kwa kamati kuu ya
taifa ya TASCA kwa ajili ya kuweka kumbukumbu na kuzihakikisha kama ni za kweli.

No comments
Post a Comment