Zinazobamba

ZITTO KABWE AMZIMA SAMSON MWIGAMBA NA KUNDI LAKE,SOMA HAPO KUJUA

ZITTO Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, ameeleza masikitiko juu uongo uliotumiwa na walikuwa wafuasi wa chama hicho, Samson Mwigamba na wenzake kuwa chama hicho kimekiuka misingi iliyojiwekea, anaandika Faki Sosi.
Zitto ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi Kuu za Chama hicho ambapo amesema kuwa Mwigamba hajaweka wazi misingi ambayo chama hicho kimekiuka hatimaye akatangaza kutimka.
“Kutokana na unyeti wa madai haya, kikao cha Kamati ya Uongozi kiliitishwa na mtoa madai alipewa mwaliko ili aweze kufafanua jinsi misingi au msingi wa chama anaodhani umevunjwa,” amesema Zitto.
Zitto ameongeza: “Tulifanya hivi kwa sababu tangu kuasisiwa kwake, chama cha ACT-Wazalendo kimejipambanua kuwa chama kinachosimamia misingi.
“Licha ya kutumiwa mwaliko, mtoa madai hakuhudhuria kikao cha Kamati ya Uongozi na badala yake kuitisha mkutano na waandishi wa habari ambapo alitangaza kujiuzulu uanachama kwa madai ya kuunga mkono juhudi za serikali ya sasa.”
Zitto amesema kuwa chama hicho kimejitathmini na kujiona bado kipo kwenye misingi imara iliyojiwekea ya kiokombozi kwenye masuala mbalimbali ya kitaifa.