Zinazobamba

RAIS MAGUFULI AENDELEA KUWAPA "SHAVU" WANAWAKE WA VIGOGO WA CCM,,AMPA NAFASI HUYU PIA,SOMA HAPO KUJUA


RAIS John Magufuli ameendelea kuwateua na kuwapa nafasi za Ubunge wa Viti Maalum wake wa viongozi wastaafu wa Chama cha Mapinduzi ,baada ya kumteua Janeth Masaburi kuwa Mbunge wa Viti Maalum.Anaandika Karoli Vinsent endelea nayo.

Janeth Masaburi ambaye ni Mke wa Mrehemu Dk Didas Masaburi  ambaye alikuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam,ameteuliwa na Rais Magufuli ambapo teuzi huo kwa mujibu wa Ibara ya 66 (1)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayompa mamlaka ya kuteua wabunge 10 watakaokuwa miongoni mwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Janeth Masaburi anakuwa pia ni miongoni mwa wake wa viongozi waastaafu kupata nafasi hiyo,baada ya Rais Magufuli Kumteua Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete Mama Salma Kikwete pamoja na Mke wa John Malecela ,Anne Malecela kuwa Mbunge wa Bunge hilo.