Zinazobamba

MWALIMU WA SEKONDARI AJIUUA KINYAM KWA WIVU WA MAPENZI,SOMA HAPO KUJUA



Leonard Mwipugi (29) ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Mtenga wilayani Nkasi, amejiua kwa kujichinja koromeo akiwa nyumbani kwake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio Mratibu wa Elimu Kata ya Mtenga, Hebron Mwafungo amebainisha kwamba Mwipugi amekutwa akiwa amekufa baada ya kujichinja.

Amefafanua kuwa marehemu amafanya kitendo hicho nyumbani kwake jana  saa sita mchana.

Aidha Mwafungo amesema kabla ya mwalimu huyo kukutwa amejiua, alikwenda kazini kwake na saa 5 alirejea nyumbani ambapo hakumkuta mkewe.

Ameelza  baada ya muda walipata taarifa kuwa mwalimu huyo amekutwa amekufa baada ya kujichinja koromeo akiwa chumbani kwake.

Amebainisha kwamba licha Mwipugi kuishi na mkewe alikuwa pia akiishi na mdogo wake na wakati wa tukio hilo alikuwa  amemtuma mbali kidogo ya nyumbani.


Hivyo baada ya mdogo huyo kurudi aliona damu zikichuruzika na alipochungulia chumbani alikuta kaka yake amekwishafariki.