TIGO, TAMOSA WAJIKITA KUWANASUA BODABODA, WANDAA UZINDUZI YA MPANGO SALAMA WA BODABODA, PINDA KUWA MGENI RASMI
AFISA HABARI WA KAMPUNI YA MAWASILIANO YA TIGO,JOHN WANYANCHA AKIFAFANUA
JINSI KAMPUNI YA TIGO ILIVYOJIKITA KATIKA KUFANIKISHA UZINDUZI WA
MPANGO SALAMA WA HUDUMA SALAMA WA USAFIRI WA BODABODA KITAIFA
UTAKAOFANYIKA HIVI KARIBUNI MJINI DODOMA, KATIKA UZINDUZI HUO MGENI
RASMI ANATARAJIWA KUWA WAZIRI MKUU WA TANZANIA MH. MIZENGO KAYANZA PETER
PINDA
Kampuni ya mawasiliano ya Tigo hapa nchini leo hii imetangaza nia yake ya kudhamini shughuli zote za Tamosa zinazopelekea uzinduzi wa mpango wa usafiri salama wa bodaboda hapa nchini ili kuongeza ufanisi katika sekta ya usafiri kwa kupitia bodaboda,
Akizunguzungumza na waandishi wa habari, mapema hii leo, Afisa habari wa kampuni hiyo, amesema wameamua kuingia na kufadhili hatua zote za uzinduzi wa mpango wa usafiri salama wa boda boda wakijua wazi kuwa kufanya hivyo kutasaidia jamii wanaofaidika na usafiri huo kutumia usafiri huo kwa raha bila kuvunja taratibu za nchi,
Amesema wazo la kuratibu shughuli zote za wanabodaboda hapa nchini si la kupuuzwa hata kidogo ikizingatiwa kuwa kwa sasa biashara hiyo inakuwa kwa kasi huku uratibu wake ukionekana mgumu sana kwa idara mbalimbali kuufanikisha,
Amesema wao kama kampuni ya Tigo, wanaamini kuwa uratibu mzuri wa shughuli za usafiri wa Bodaboda utaongeza ufanisi wa biashara na hata fujo katika miundombinu yetu itapuungua kwa kiasi kikubwa sana,
Naye, mkuu wa wakala wa usafiri wa bodaboda hapa nchini, amesema wameamua kuja na wazo la kuratibu shughuli zote za usafiri wa bodaboda ili kuleta majibu ya wanabodaboda wanoanekana ni kero katika majiji mbalimbali hapa nchini,
Akizuungumzia hatua iliyochukuliwa na serikali ya kuwazuia wana bodaboda kuingia katikati ya jiji kufanya biashara zao, afisa huyo amesema kuwa, utaratibu ambao serikali wameutumia wafanyabiashara wa bodaboda ni wa kikatili sana na kwamba ingekuwa yeye ndio muamuazi angependa wafanyabiashara hao waendelee kutoa huduma ndani ya jiji
Kama hoja ya kuleta foleni katikati ya jiji haona mashiko hata kidogo kwani magari ya watu binafsi kwa kiasi kikubwa yanaoonekana kuongeza foleni kuliko hizo bodaboda, sasa iweje leo bodaboda ionekane ni sababisho la foleni katikati ya jiji,
Amesema yeye kama wakala wa usafiri salama wa bodaboda, anawaunga mkono wanabodaboda, na kwamba suala la madai kuwa wanasababisha uharifu katikakti ya jiji sio kweli kwani kama kuna uratibu mzuri ni rahisi hata kuudhibiti huo uharifu, aliongeza afisa huyo
No comments
Post a Comment