SIKU 100 ZA RAIS DKT.SAMIA MADARAKANI KATA YA KISUKURU YAPIGA HATUA KUBWA SEKTA YA ELIMU,AFYA,ULINZI NA UTAWALA BORA.
Na Musaa Augustine.
Kata ya Kisukuru Jijini Dar es salaam imefanikiwa kupiga hatua kubwa katika Sekta za Elimu,Afya,Utawala Bora,Ulinzi na usalama pamoja na Biashara katika kipindi cha siku miamoja ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan madarakani.
Hayo yamesemwa leo Januari 26,2026 na Diwani wa kata hiyo Mh.Lucy Lugome wakati akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake nakubainisha kuwa siku miamoja za Rais Dkt Samia zimekua za mafanikio makubwa ya maendeleo kwenye kata hiyo.
"Tumejaribu kuangalia nakuona matokeo ya miaka mitano ya nyuma 2025,ufaulu ulikua ukipanda na kushuka,sasa tukaona awamu hii tumerudi tena 2025/2030 na rais wetu Dkt. Samia yupo madarakani na mkakati wake wa siku miamoja,tukaona na sisi tutumie siku hizi kuweka mkakati katika kupunguza ziro kwenye shule yetu" amesema Mh.Lugome
Nakuongeza kuwa "Ufaulu wa wanafunzi umeonekana haujakaa vizuri sana unapanda na kushuka,sisi kwa kawaida tunaona bora kutokomeza ziro kabisa,na kama kuna Division four ( ufaulu daraja la 4)nazo ziweze kupotea ili shule zetu za Serikali ziweze kufanya vizuri."
Aidha amesema kuwa yeye kama diwani wa kata ya Kisukuru kwa kushirikiana na kamati ya maendeleo ya kata hiyo,wameanza mkakati huo kwa kuanza kufanya kikao na Wazazi wa wanafunzi wa kidato Cha pili nacha nne( form two na form four) pamoja na walimu nakuweza kufikia madhimio ya kuweza kuongeza ufaulu wa wanafunzi hao.
"Nikiwa kama diwani nilionesha mfano wa kuigwa baada ya kuchangia fedha za mitihani yote ambayo itafanyika wiki hii,nitasimamia kwa gharama zote nakuona wiki ya mwisho ya kufunga mwezi januari watoto wameweza kufanyaje nikiwa kama kiongozi wao" amesema Diwani huyo.
Aidha amesema kuwa,walimu pia walikua na mkakati wa kuweza kutafuta matokeo ya kila mwezi ya wanafunzi wa kidato cha pili na kidato cha nne,ili kuangalia madaraja ya ufaulu kuanzia daraja la kwanza hadi mwisho(Division one hadi Division 0) hali ambayo itasidia wanafunzi kuwa na hali ya kujiamini wakati wa kufanya mitihani ya kidato cha nne.
"Pia tumegundua changamoto kubwa ya kukosekana kwa ulinzi kwa watoto shuleni,utoro umekua mkubwa sana,watoto wanafanya mambo ambayo sio mazuri, wengine wanavuta bangi, kwahiyo tumeongea na wenzetu wa jeshi la Polisi kata ili tuweze kufanya doria ya kila wiki kwenye shule yetu na kutoa elimu kwa wanafunzi ili kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake."amesema
Kuhusu Sekta ya Afya Diwani huyo amesema kuwa upande wa Afya wanamshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwasababu kuna mchakato mkubwa wa kujenga hospitali ya ghorofa tatu itakayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 5.
"Kata yetu ya Kisukuru tunakwenda kujenga hospitali ya ghorofa tatu,hospitali hii tayari mchakato wote umekamilika na fedha zilikuepo shilingi bilioni 5.mwaka 2025,lakini mwaka 2025/30 hospitali hii itajengwa rasmi."amesema.
Nakuongeza," Mimi binafsi niseme nilikua nikitoa bima za Afya kwa Wananchi wangu wajumbe wa mashina sababu wanafanya kazi kubwa sana, lakini nilipoona hili jambo la bima ya Afya kwa wote limewekwa vizuri sana na Rais wetu,naahidi kulifanyia kazi na kulisimamia kwa asilimia 100%, nitafanya mwendelezo mzuri kumsaidia Rais Dkt.Samia.
Akizungumzia kuhusu Utawala bora amesema kuwa katika siku miamoja za Dkt.Samia madarakani wamepata jengo lao halali la Serikali,ambapo hapo awali ofisi za kata zilikua kwenye jengo la kupanga,na sasa wametoka kupanga na kumiliki jengo la Serikali,hali ambayo itawezesha kufanya kazi kwa weledi zaidi.
Kuhusu Mikopo ya asilimia 10 amesema kwamba,Kata ya Kisukuru kuna mikopo ilitolewa kipindi cha nyuma kuanzia 2017 lakini haikufanya vizuri,lakini kwa kipindi hiki cha siku mia moja za mama (Rais Dkt.Samia) ameonesha ni jinsi gani anataka kufanya kazi na Wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu,hivyo wameitana kama baraza la kata kwa ajili ya kujadili namna ya kusaidia jambo la mikopo liende vizuri.
"Wale ambao walichukua mikopo kipindi cha nyuma waweze kufanya marejesho yao kwa kiasi kadri siku zinavyoenda ikifika mwezi tuone angalau kiasi fulani kimekusanywa." Amesema
Nakuongeza"pia kwenye mikopo mingine ambayo imetolewa,mimi najivunia kwenye kata yangu kuna baadhi ya mitaa Vijana wetu wa bodaboda wameweza kupata mkopo wa bodaboda,vipo vikundi takribani viwili vimeweza kupata bodaboda ndani ya siku hizi miamoja za mama(Rais Dkt.Samia) kwahiyo tunaona mama ameahidi na ameweza kutekeleza."
Hata hivyo ameomba mikopo hiyo iwanufaishe zaidi Wajasilimari wadogowadogo zaidi ikiwemo wakina mama wanaouza mboga mboga,karanga,mihogo,matunda,Vijana wanaouza matunda na mkaa.
Aidha amesema kabla ya kutamatika kwa siku miamoja za Rais Dkt Samia madarakani anatarajia kufanya tamasha la kuhamasisha Wanawake na Vijana kupeana elimu ili mikopo hiyo ielekee kwa makundi hayo ili kupata watu wengi wenye uwezo wa kufanya kazi kwa fedha zinazotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


No comments
Post a Comment