Zinazobamba

WAKILI MASOUD AMEIOMBA SERIKALI KUHESHIMU MAAMUZI YA MAHAKAMA.


Na Mwandishi Wetu.

Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Kisheria cha Everlasting Legal Aid Foundation(E.L.A.F)wakili Khamisi Masoud,ameiomba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na watumishi wake kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia misingi ya Katiba na Sheria za nchi na kuheshimu maamuzi ya mahakama.

Wakili huyo amesema hayo leo Januari 26, 2026, jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kufuatia mgogoro wa ardhi kati ya Paulina Ndungule na Pili Kafuye ulioanza mwaka 2015 na mahakama kutoa hukumu ya kesi hiyo ambapo Paulina Ndungule ameonekana kua ni mmiliki halali wa eneo hilo.

 Wakili Masoud amesema serikali ipo kwa ajili ya kusimamia sheria,na kwamba kiongozi yeyote anayekiuka amri ya mahakama ni kuvunja uhalali wake wa kimaadili na kuhatarisha misingi ya utawala wa sheria.

“Mahakama inapotoa uamuzi kwamba haki ni ya mtu fulani,basi madai na jinai ni mambo mawili tofauti,katika mgogoro wa ardhi,mahakama ilishathibitisha nani mmiliki halali."amesema

Nakuongeza," Mtu kujipa mamlaka kudharau maamuzi ya wazee wa kimila hadi Mahakama Kuu ni jambo hatari kwa taifa,Serikali ikiruhusu hali hii,wananchi wataidharau mahakama na kuamini kuwa nguvu zipo kwa watu binafsi badala ya sheria."

Aidha ameendelea kusema kwamba kutoheshimiwa kwa maamuzi ya mahakama kunachochea ghasia,chuki na vurugu katika jamii,na hatimaye kujenga utawala wa watu wenye nguvu kuliko sheria,jambo linaloathiri amani na haki nchini.
Kwa upande wake,Msimamizi wa Mirathi, Zawadi James,amesema mgogoro huo wa ardhi ulianza mwaka 2015 kati ya Paulina Ndungule na Pili Kafuye nakubainisha kuwa marehemu Paulina Ndungule ndiye aliyefungua kesi katika Baraza la ardhi kata na kushinda.

Zawadi amesema Pili Kafuye alikata rufaa kwenda Mahakama Kuu,lakini Paulina Ndungule aliendelea kushinda kesi hiyo.

 Amedai kuwa wakati kesi ikiendelea Mahakama Kuu,Pili Kafuye alianza kujenga kwenye eneo lenye mgogoro lenye ukubwa wa hekta tano na nusu, ambapo alijenga kwenye eneo la hekta moja na nusu,hali iliyozidisha mgogoro kati ya pande hizo mbili.

Ameongeza kuwa baada ya hukumu ya Mahakama Kuu,Pili Kafuye alikata rufaa kwenda Mahakama ya Rufaa ambayo ni mahakama ya mwisho nchini,Mahakama hiyo pia ilitoa hukumu ikimtaka Pili Kafuye aondolewe katika eneo hilo na kulikabidhi kwa msimamizi wa mirathi.
Nae Sebastian Mathias,ambaye alikuwa shahidi wakati wa mauziano ya kiwanja hicho,amesema kuwa muuzaji halali wa kiwanja hicho alikuwa mjomba wake anayefahamika kwa jina la Mpendakula.

No comments