Zinazobamba

CUF YAWASIHI WANACHAMA WAKE NA WANANCHI KWA UJUMLA KUACHA KUBAGUANA.

*Yafanaya dua ya kuwaombea Wanachama waliofariki katika maandamano ya kisiasa mwaka 2001 Zanzibar.

Na Mussa Augustine.

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi(CUF)Taifa Profesa Ibrahim Lipumba amewasihi wanachama wa Chama hicho pamoja na Wananchi kwa ujumla kuacha kubaguana kwa misingi ya udini, Uzanzibari na Utanganyika. 

Profesa Lipumba amesema hayo leo Januari 27,2026 wakati wa dua ya kuwaombea wanachama wa chama hicho waliopoteza maisha kwenye vurugu za maandamano ya kisiasa Januari 27, 2021 yaliyofanyika Pemba Visiwani Zanzibar ambapo watu takribani 71 walipoteza maisha.

Aidha amesema migogoro ya kisiasa imekua ikisababishwa na baadhi ya viongozi wa chama cha siasa hapa nchini (jina kapuni) na moja ya taasisi, kutokana na madai ya kutangazwa matokeo yasiyo sahihi wakati wa uchaguzi mkuu, hivyo hali hiyo isiwafanye Watanzania wabaguane kutokana na dini. 
"Tusikubali kugawanyika kidini,tusiingie kwenye mtafaruku wa aina yoyote,kwani waliotugawa kisiasa wanajulikana  kwa kupitisha wagombea ambao hawajachaguliwa na wananchi". Amesema Prof. Lipumba. 

Nakuongeza "sisi CUF ni chama ambacho kinasimamia umoja wa Kitaifa,chama kinahakikisha Wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar wanapata haki sawa bila kuwepo ubaguzi wa aina yoyote". 

Aidha amewambia Wananchama wa CUF kuwapuuza wale wanaokuja na agenda ya kudai kuwa wanachukiwa kwasababu ni Wazanzibar,nakwamba migogoro yote ya ly isuluhishwe kwa amani.

Ameongeza kuwa Chama Cha CUF, kitaendelea kusimamia umoja,amani kwa Watanzania wote bila kujali utofauti wa dini na kisiasa na kuwataka watanzania kukataa agenda ya kubaguana.

Amesisitiza kuwa matatizo katika nchi yanapotokea ni vyema yakatatuliwa kwa njia ya amani na utulivu ili kuendelea kujenga misingi ya amani na utulivu.

Ikumbukwe kuwa Januari 27 ya kila mwaka(CUF )inaadhimisha mauaji ya wanachama wa CUF waliouawa tarehe 26 na 27 katika maandamano wakidai uchaguzi wa Zanzibar wa mwaka 2000 urejewe,kudai katiba mpya ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Tume huru ya uchaguzi,Utawala bora wenye misingi ya kufuata Sheria. 


No comments