BODABODA SASA KWISHA HABARI YAO, JESHI LATANGAZA MIPAKA , WAKIVUKA TUU WANALO
POLISI, SUMATRA,
NA HALMASHAURI KUENDELEZA OPARESHENI YA KUZUIA PIKIPIKI NA BAJAJI
KATIKA ENEO LA CBD

Jeshi la Polisi Kanda Maalum D’Salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya utawala linaendelea na mpango kamambe wa kukamata pikipiki (bodaboda) na bajaji kutoingia katikati ya jiji ikiwa ni kutekeleza sheria zilizopo. Hii ni kutaka kuhakikisha kuwa jiji la Dar es Salaam kuna usalama wa kutosha ikiwa ni pamoja na kutii sheria za usalama barabarani.
Oparesheni hii ni mahsusi kwa mujibu wa sheria ijulikanayo kama “THE TRANSPORT LICENCING (MOTORCYCLES ANDTRYCYCLES) REGULATIONS, 2010” inayozuia vyombo hivi kuingia CBD. Kwa jiji la Dar es Salaam, maeneo yanayoishia CBD ni kama ifuatavyo:

- TEMEKE – Maungio ya barabara ya Mandela na Kilwa Road.
- KINONDONI – Mwenge (barabara ya Ally Hassan Mwinyi), Daraja la Mlalakuwa (barabara ya Mwai Kibaki “Old Bagamoyo”, na Ubungo (barabara ya Morogoro).
- ILALA – Tazara (Barabar ya Nyerere)
No comments
Post a Comment