taarifa ya tigo kwa waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa mpango salama
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Tigo
yadhamini mpango wa kupunguza ajali za bodaboda nchini
Dar es Salaam, 18
Machi 2014
– Tigo Tanzania imetangaza kushirikiana na taasisi ya usalama wa pikipiki
nchini katika kuzindua Mpango wa Huduma Salama ya Usafiri wa Bodaboda Kitaifa
itakayofanyika mjini Dodoma, 23 Machi, 2014.
Akizungumza katika mkutano na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam, iliyowashirikisha pia wakala wa usalama wa
pikipiki nchini (TAMOSA), Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha, alisema kwamba
udhamini wa Tigo katika mpango huo wa kitaifa wa usalama wa bodaboda nchini ni
ishara ya kwamba kampuni hiyo ya simu inajali na kufuatilia kwa karibu kuhusu
masuala ya usalama barabarani nchini.
“Wote
ni mashuhuda wa jinsi biashara hii ya pikipiki ilivyoweza kushamiri ndani ya
muda mfupi nchini. Kupitia bodaboda na bajaji vijana wetu wameweza kujiajiri
wenyewe na kuweza kujipatia kipato kinachowasaidia kumudu maisha,” alisema
Wanyancha.
“Lakini
kila kitu huja na changamoto zake, na katika hili suala la ajali barabarani limekuwa
dosari kubwa. Kama kampuni, tuliamini kwamba hii itakuwa fursa nzuri kwa sisi
kama wadau kujaribu kuhamasisha kuhusu usalama barabarani kwa ajili ya kusaidia
kupunguza idadi ya ajali zinazotokea huku tukihakikisha kwamba sekta hii
inaendelea kuwa chachu ya ajira kwa vijana nchini,” alisema.
Kutokana na maelezo ya Mratibu wa
Matukio kutoka TAMOSA, Kizito Msangya, alisema kwamba uzinduzi wa mpango huo wa
usalama utafanyika kwa njia ya maandamo ya amani kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa
mpaka Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ambapo Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda
ndio atakuwa mgeni rasmi.
“Tunatarajia mamia ya wamiliki na waendesha
pikipiki kutoka nchini kote kufika katika tukio hili. Ukiondoa mbali na Mheshimiwa
Pinda, pia tunatarajia Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe, wabunge
pamoja na mamlaka za usalama barabarani kushiriki katika uzinduzi huu,” alisema
Msangya.
Ripoti za Polisi zinaonyesha kuwa
kumekuwa na ongezeko la matukio 264 ya ajali
barabarani kwa mwaka 2013 sawa na asilimia
1.1 tofauti na mwaka 2012 ambapo matukio
yalikuwa 23,578.
Takwimu pia zinaonyesha kuwa walioathirika zaidi
na ajali za barabarani kwa mwaka 2013 ni waenda kwa miguu, abiria,
waendesha pikipiki, wapanda baiskeli, madereva pamoja na wasukuma mikokoteni.
Ambapo kati ya makundi hayo, ajali za pikipiki zimeongoza kwa ajali
nyingi, kwa mwaka 2013 ajali zilikuwa 6,831 sawa na ongezeko la asilimia 18.5 ya
ajali 5,763 zilizotokea mwaka juzi.
Mwisho.
Kuhusu Tigo:
Tigo ni mtandao wa kwanza wa simu za mkononi
nchini Tanzania. Ilianza shughuli mwaka 1994 na inapatikana katika mikoa
thelathini (30) Tanzania bara na visiwani.
Lengo la Tigo ni kuwa mtandao unaoongoza kwa
kutoa huduma bora na za ubunifu Tanzania kwa wateja wake wote ambazo zinaendana
na mahitaji yao kuanzia huduma za sauti za bei nafuu, vifurushi vya intaneti
vyenye kasi kubwa na huduma bora za fedha za simu za mkononi kupitia Tigo Pesa.
Tigo ni sehemu ya kampuni kubwa ya Millicom
ambayo ni ya unafuu wa huduma na inapatikana kirahisi kwa zaidi ya wateja milioni 47 katika masoko
13 barani Afrika na Amerika ya Kusini.
"Tabasamu upo na Tigo." Kwa taarifa zaidi tembelea www.tigo.co.tz
Au
wasiliana na: John
Wanyancha – Meneja Mawasiliano Tigo
Simu: +255 658 123 089 john.wanyancha@tigo.co.tz
No comments
Post a Comment