Zinazobamba

SABABU ZA KUFUKUZWA ASKARI WANNE KWA IABU NDANI YA DARESALAAM ZABAINIKA, NI KUTOKANA NA KAMPUNI YA KICHINA HONG YANG KUJA JUU


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA



jeshi la polisi


PRESS RELEASE
17/03/2014


ASKARI WANNE (4) WA JESHI LA POLISI WAFUKUZWA KAZI KWA FEDHEHA KWA KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA UHALIFU
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewafukuza kazi kwa fedheha askari wanne wa Jeshi la Polisi kutokana na makosa ya kujihusisha na vitendo vya uhalifu. Askari waliofukuzwa wanatoka katika vikosi mbalimbali kama ifuatavyo:
  • E.6396 CPL RAJABU MKWENDA @ UGORO wa Makao Makuu ya Polisi.
  • F.9412 PC SIMON wa Kituo cha Polisi Kati.
  • F.9414 PC ALBERNUS KOOSA wa Kikosi cha Bendi ya Polisi D’Salaam
  • F.9512 PC SELEMAN wa Kituo cha Polisi Kigamboni
Uchunguzi wa awali umeonyesha kwamba askari hao wamekuwa wakijihusisha na uhalifu ikiwa ni pamoja na tukio la tarehe 09/03/2014 eneo la Mbezi Beach “A” ambapo majambazi wapatao 15 walifika katika ofisi ya Kampuni ya Kichina ijulikanayo kwa jina la HONG YANG inayojishughulisha na ujenzi na uselemala.
Katika tukio hilo majambazi wapatao 11 wakivamia ofisi hiyo majira ya saa 04:30 Asb, na kupora vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja fedha taslim, simu, n.k. na kutoweka.
Imegundulika kwamba baadhi ya majambazi hai ni askari Polisi. Uchunguzi wa kina umefanyika na watuhumiwa hao 11 wamepatikana ndipo ilipobainika kwamba askari Polisi hao walishiriki katika tukio hilo.
Watuhumiwa wengine saba wa ujambazi waliokamatwa ni hawa wafuatao:
  • GERADI S/O RAJABU MTUTU, Miaka 36, Mfanya biashara, mkazi wa Mtoni Mtongani.
  • CHARLES S/O HIZA MBELWA, Miaka 37, Fundi magari, Mkazi wa Kurasini.
  • ADAM S/O MKOMBIZI MOHAMED, Miaka 40, Mkazi wa Kariakoo.
  • ALLY S/O RASHID SALUM, Miaka 38, Mkazi wa Vingunguti Spenco.
  • SALUM S/O ABDUL MUSSA, Miaka 22, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mbagala Kuu.
  • JUMA S/O SAID HAMIS, Miaka 29, Mkazi wa Yombo kwa Limboa.


  • JUMA S/O OMARI NGWELE, Miaka 50, Mfanyabiashara Samaki Ferry, Mkazi wa Mbagala Kimbangulile.

Watuhumiwa wote hao wametambuliwa na mashahidi mbalimbambali katika tukio hilo. Kabla ya kufukuzwa kazi, askari hao walishtakiwa katika mahakama ya kijeshi na walipatikana na hatia hivyo wamepewa adhabu ya kufukuzwa kazi kwa kosa la kulifedhehesha Jeshi la Polisi. wamefukuzwa kazi kuanzia tarehe 17/03/2014 na sasa si askari tena bali ni raia wa kawaida.
Aidha jalada la kesi hiyo pamoja na majalada mengine ya kesi ya wenzao waliowataja yatapelekwa kwa mwanasheria wa Serikali hivi karibuni kabla ya kuwafikisha mahakamani kwa makosa jinai.
Pamoja na malezo hayo, Jeshi la Polisi halitavumilia vitendo vya ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa Jeshi la Polisi na hatua hizi ni fundisho kwa askari wa cheo chochote atakayejaribu kwenda kinyume cha taratibu na maadili ya kazi.
Jeshi la Polisi litaendelea kuwazawadia askari wenye kufanya vitendo vya ujasiri vinavyoendena na tabia njema kama ilivyofanyika hivi karibuni tarehe 07/03/2014. Pia Jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu maafisa, wakaguzi na askari watakaokiuka maadili au kukiuka mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi (Good Conduct)


POLISI, SUMATRA, NA HALMASHAURI KUENDELEZA OPARESHENI YA KUZUIA PIKIPIKI NA BAJAJI KATIKA ENEO LA CBD
Jeshi la Polisi Kanda Maalum D’Salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya utawala linaendelea na mpango kamambe wa kukamata pikipiki (bodaboda) na bajaji kutoingia katikati ya jiji ikiwa ni kutekeleza sheria zilizopo. Hii ni kutaka kuhakikisha kuwa jiji la Dar es Salaam kuna usalama wa kutosha ikiwa ni pamoja na kutii sheria za usalama barabarani.
Oparesheni hii ni mahsusi kwa mujibu wa sheria ijulikanayo kama “THE TRANSPORT LICENCING (MOTORCYCLES ANDTRYCYCLES) REGULATIONS, 2010” inayozuia vyombo hivi kuingia CBD.
Kwa jiji la Dar es Salaam, maeneo yanayoishia CBD ni kama ifuatavyo:
  • TEMEKE – Maungio ya barabara ya Mandela na Kilwa Road.


  • KINONDONI – Mwenge (barabara ya Ally Hassan Mwinyi), Daraja la Mlalakuwa (barabara ya Mwai Kibaki “Old Bagamoyo”, na Ubungo (barabara ya Morogoro).


  • ILALA – Tazara (Barabar ya Nyerere)
Aidha, lazima ieleweke kwamba vyombo hivi vya usafiri (pikipiki na bajaji) hawajakatazwa kufanya biashara ila hawaruhusiwi kuingia katikati ya mji na wanaruhusiwa kufanya biasharkwa mujibu wa sheria.a maeneo ya nje ya mji kama ilivyoainishwa

KUPATIKANA KWA SILAHA MBILI AINA YA BASTOLA
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limefanikiwa kukamata Bastola moja aina ya Browning yenye namba Z. 27977 ikiwa na risasi nne ndani ya magazine. Bastola hiyo ilikamatwa tarehe 19/02/2014 huko maeneo ya Tandika Azimio (W) Temeke jijini Dar es Salaaam, baada ya Polisi kupata taaarifa toka kwa ulinzi shirikishi wa eneo hilo kuwa kuna mtu mmoja aitwaye Abdul s/o Hassan @ Mudo, miaka (22), mkazi wa Tandika anamiliki silaha hiyo.
Baada ya taarifa hiyo kikosi kazi cha Polisi Chang’ombe kwa kushirikiana na ulinzi shirikishi na kwa umakini wa hali ya juu, waliweka mtego eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwana alipopekuliwa alikutwa na bastola hiyo kiunoni. Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mtuhumiwa huyo ni jambazi mzoefu na ameshiriki katika matukio mbalimbali ya ujambazi hapa jijini. Upelelezi wa shauri hili unandelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu shtaka linalomkabili.


Katika tukio lingine mnamo tarehe 12/3/2014 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata silaha moja aina ya bastola ya kichina yenye namba 618395SA ikiwa na magazine ambayo haikuwa na risasi. Aidha risasi tatu zilikuwa zimefungwa katika vitambaa viwili vyekundu huko maeneo ya Kongowe njia panda Kigamboni katika kituo cha mafuta Oil Com.
Askari walipata taarifa kutoka kwa msiri kuwa kuna majambazi wapatao watatu wakiwa na silaha wamepanga kufanya uporaji wa pesa katika kituo cha mafuta Oil Com. Askari waliweka mtego huo na kufanikiwa kuwakamata majambazi wawili ambao ni AHMAD S/O YUSUPH, Miaka 19, na IDRISA S/O OMARY @ CHASIMBA 18, dereva wa bodaboda, mkazi wa Mbagala Charambe. Aidha majambazi hao walikutwa na makoti mawili rangi ya chungwa, kofia moja ya kapero rangi nyeupe, leseni ya udereva, kitambulisho cha Charambe Boxing Club na simu moja ya mkononi aina ya Itel.
Majambazi hao wanashikiliwa na Polisi kwa mahojiano zaidi huku msako mkali ukiendelea wa kumtafuta jambazi mwingine mmoja aliyekimbia na silaha.


KUKAMATWA KWA BUNDUKI AINA YA MARK IV, PIKIPIKI MOJA NA MTUHUMIWA MMOJA.
Katika hatua nyingine, jeshi la Polisi Kanda Maalum limekamata bunduki moja aina ya MARK IV, pikipiki moja pamoja na mtuhumiwa aliyejitambulisha kwa jina la RAJABU S/O SAIDI, Miaka 34, Fundi magari, mkazi wa Tandale Magharibi.


Hii ni baada ya polisi kuitilia mashaka pikipiki hiyo iliyokuwa imebeba watu wawili na kuisimamisha. Abiria aliyekuwa amebebwa katika pikipiki hiyo alikimbia baada ya kusimamishwa lakini dereva wa pikipiki hiyo alitiwa mbaroni na alipopekuliwa alikutwa na bunduki hiyo iliyokuwa ndani ya begi ambayo imekatwa mtutu na kitako ikiwa haina risasi. Bunduki hiyo ilikuwa imefichwa katika kiti cha pikipiki hiyo.


Aidha, pikipiki iliyokamatwa ni yenye namba T742 CKH aina ya SunLG, rangi nyekundu ambayo inashikiliwa katika kituo cha polisi Kimara pamoja na mtuhumiwa ambaye anaendelea kuhojiwa kuhusiana na umiliki wa Bunduki hiyo.









KUPATIKANA KWA TINDIKALI LITA ISHIRINI NA MOJA
Jeshi la Polisi Kanda Maalum D’Slaam limefanikiwa kukamata kemikali inayoaminika kuwa ni Tindikali yenye ujazo wa lita ishirini na moja (21) iliyokuwa imehifadhiwa katika madumu mawili ya plastiki, moja la lita ishirini (20) na dumu dogo la lita moja. Tukio hili limetokea mnamo tarehe 23/02/2014 huko maeneo ya Vingunguti Miembeni, (W) Ilala, jijini Dar es Salaam, katika chumba cha mtu mmoja mpangaji aliyejulikana kwa jina KILOGO S/O ALEN ambaye hakuwepo chumbani hapo wakati huo.
Awali zilipokelewa taarifa katika kituo cha Polisi Vingunguti toka kwa walinzi shirikishi wa eneo la Vingunguti Miembeni na ndipo askari walipoamua kufutilia katika nyumba husika na kufanikiwa kuipata kemikali hiyo ambayo kwa sasa imehifadhiwa kituo cha Polisi Vingunguti na upelelezi unaendelea ili kumtambua na kumkamata muhusika wa kemikali hiyo.
Aidha tunapenda kuwashauri wananchi kuchukua tahadhari kuhusu kemikali ambayo hawana uhakika na matumizi yake kwa kuwa zina kemikali nyingine zina madhara ya moja kwa moja kwa binadamu na mazingira.


S. H. KOVA – CP
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

No comments