Zinazobamba

HUYU NDIYE MWENYEKITI WA CHADEMA ALIPIGWA NA WAFUASI WA CHADEMA WAKIMTUHUMU KUSHILIKIANA NA ZITTO KABWE KUKILARUA CHAMA

Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Temeke Joseph Yona amepigwa na watu wasiojulikana na kisha kutupwa kwenye eneo la Ununio kwenye Magorofa ya Wasomali Kawe Dar es salaam.

 
Shuhuda Abdul Ally ambae ni mkuu wa nyumba zilizokaribu na alikopigwa Mwenyekiti huyu, anasema walisikia kelele za huyu mtu kupigwa saa tisa usiku na walipomsogelea walimkuta peke yake.
 
‘Niliomba wasiniue, wamenipiga sana… wamenichukua saa tano nyumbani kwangu Kwa Aziz Ally, wao walikua na gari kama ya Polisi lakini inaonekana sio ya polisi wakasema tunakupeleka Central, tulikua wanne na hawakuhangaika na mtu wakanichukua mimi moja kwa moja.. tulipopanda kwenye gari wakachukua nguo yangu wakanifunga uso, wakaanza kunipiga wakisema nisiwajibu na hawakuniambia chochote’
 
KAMISHINA WA POLISI KANDA MAALUM YA DARESAALAAM AKIWA KATIKA MOJA YA MIKUTANO YAKE NA WAANDISHI WA HABARI, picha na maktaba yetu
 
Unaweza kusikiliza maelezo yake mengine akihojiwa kwa kubonyeza play hapa chini..
 
KAMANDA KOVA AONGEA NA WAANDISHI JUU YA SAKATA HILO NA KUWEKA KILA KITU HADHALANI

Hapa mwandishi wa blog hii Ndg. Vicent Karoli anashuka nayo......

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimeingia kwenye kashfa nzito baada ya kuhusishwa kwenye utekaji wa Mwenyekiti wa Chadema  wilaya ya Temeke Ndg Joseph Yona.

Taarifa toka ndani ya jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ambapo mwandishi wa mtandao huu amezipata baada ya kuthibitishwa na Kamisha wa kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova Mbele ya Waandishi wa Habari leo Zinasema Jeshi hilo la polisi linafanyia uchunguzi wa kina kuhusu tukio la kutekwa nyara ,kupigwa na kujeruhiwa na hatimaye kutupwa vichakani dhidi  ya mtu anaitwa Joseph Yona miaka 32 mkazi wa Temeke mtoni kwa Azizi Ally.

Taarifa hiyo inasema alitekwa na kutupwa vichakani ni mwenyekiti wa chadema  wilaya ya Temeke ambaye pia ni Mtaalam wa Maabara chuo cha Elimu (DUCE) kilichopo Changombe.

Vilevile  taarifa hiyo inafafanua  mnamo tarehe 7 mwezi huu saa 5 usiku eneo la Ununio ,Bw.Joseph Yonna alienda kuaomba msaada  kwa mlinzi wa kampuni binafsi aitwaye Ismail Swalehe ili aende kituo cha polisi kuripoti baada ya kupigwa na watu sita na kumtupa huko kichakani

Ndipo milinzi huyo alikubali na kumpeleka kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Ununio,ndipo mwenyekiti huyo ndipo alipowasiliana na mkuu wa polisi kawe  ambaye alifika eneo la tukio hilo akifuatana na Rpc wa kinondoni Acp Camilius Wambura.
Maofisa wa Polisi walimuhoji Joseph Yonna  Kuhusu Majeraha aliyonayo usoni sehemu mbalimbali za mwili wake.

Ndipo mlalamikajia aliweza kujieleza kuwa yeye ni mkazi wa kwa Azizi Ally wilaya ya Temeke na kwamba ilpofika saa 5.Kamili usiki ya tarehe 6 mwezi huu alikuwa akipata kinywaji katika Grocery ya Mgumbini akiwa na wenzake watatu walikuwa wakimalizia Vinywaji.

Ghafla walitokea watu sita ambao walimtaka aende nao walijitambulisha kuwa wao ni maofisa wa Polisi katika kituo cha kati.

Ndipo  katika watu hao sita aliweza kumtambua mtu mmoja kuwa ni mwanachama mwenzake wa chadema na alipojalibu kuulizia kuhusu huyo mtu walimwingiza ndani  ya Gari aina Land Cruiser na kufunga kitambaa usoni na kuondoka naye.

Katika hatua nyingine mlalamikaji alizidi kusema waliomteka walianza kumhoji ni kwa nini anaendelea kumshabikia Zitto Kabwe wakati ni  mtu anayeharibu chama chao yaani chadema.pili  walimtaka akawaonyeshe rafiki yake ambaye anajulikana kwa jina  Habibu Mchange.ndipo walizidi kumpiga mpka wakampelekea majeraha kwenye jicho na kichwani.

Uchunguzi wa awali unaonyesha wazi kuwa tukio hili lina uhusiano wa moja kwa moja na mgogoro unaoendelea katika chama cha siasa cha chadema juu ya Zitto kabwe na wenzake.Aidha kabla ya tukio hili,mlalamikaji alikuwa anapokea simu nyingi za vitisho kutoka kwa viongozi  wa ngazi mbalimbali  wa Chadema ambao anadai anawafahamu.
Vilevile Taharifa hiyo inasema Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam  limeanza uchunguzi wa sakata hilo

Uchunguzi wa mwandishi wa mtandao huu umebaini nkuwa Habibu Mchange ni miongoni mwa watu wanaosakwa sana na wanasiasa kutokana na kuhusika katika mipango ya kukihujumu chama hicho.

Wachambuzi wa masuala ya mambo ya kisiasa waliozungumza na mtandao huu wanasema siasa za Tanzania zimekuwa hazistawi kutokana na wanasiasa wa vyama  vikuu vya upinzani kuwa na tamaa za pesa na kujionyesha kuwa wanashabikia upande mmoja wasiasa
 

No comments