TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU KUTEKWA NA KUTUPWA KICHAKANI MWENYEKITI WA CHADEMA
JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
PRESS
RELEASE
07/01/2014
MWENYEKITI
WA CHADEMA WILAYA YA TEMEKE ATEKWA
NYARA,
ASHAMBULIWA NA KUTUPWA VICHAKANI
Jeshi
la Polisi kanda maalum Dsm, linafanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio
la kutekwa nyara, kupigwa na kujeruhiwa na hatimae kutupwa vichakani
dhidi ya mtu aitwaye JOSEPH YONA miaka 32 mkazi wa Temeke Mtoni kwa
Azizi Ally. Imegundulika kwamba mtu huyo ni Mwenyekiti wa Chadema
Wilaya ya Temeke ambaye pia ni Mtaalam wa Maabara Chuo Kikuu cha
Elimu (DUCE) kilichopo Chang’ombe.
Mnamo
tarehe 7/1/2014 saa 5.00 usiku eneo la Ununio, mlalamikaji aitwaye
Joseph Yona alienda kuomba msaada kwa mlinzi binafsi aitwaye ISMAIL
SWALEHE ili aende Kituo cha Polisi kuripoti. Mlinzi alimuona Joseph
Yona akiwa katika hali mbaya ya kujeruhiwa. Aliamua kwanza ampeleke
kwa mwenyekiti wa serikali za mitaa Ununio. Mwenyekiti wa Ununio
alipopatikana aliwasiliana na Mkuu wa Polisi Kawe ambaye alifika
eneo la tukio akifuatana na RPC Kinondoni ACP. Camilius Wambura na
kundi la wapelelezi. Maofisa wa Polisi walimhoji mlalamikaji kuhusu
majeraha aliyonayo usoni na sehemu mbali mbali za mwili wake.
Mlalamikaji aliweza kujieleza vizuri kwamba yeye ni mkazi Mtoni kwa
Azizi Ally wilaya Temeke na kwamba ilipofika saa 5.oo ya tarehe
6/1/2014 alikuwa akipata vinywaji katika grocery ya Mgumbini eneo la
Mtoni kwa Azizi Ali akiwa na wenzake watatu walikuwa wakimalizia
vinywaji. Ghafla walijitokeza watu sita ambao walijitambulisha kuwa
ni Maafisa wa Polisi na walimtaka aende nao Kituo cha Polisi cha
Kati. Hata hivyo kati ya watu hao sita aliweza kumtambua mmoja wapo
kwa sura na jina (limehifadhiwa) kwamba ni mwanachama mwenzake wa
Chadema na alipojaribu kuulizia kuhusu huyo mtu aliyemtambua, haraka
walimwingiza ndani ya gari Land Cruiser na kumfunga kitambaa usoni na
kuondoka naye.
Uchunguzi
wa awali unaonyesha wazi kuwa tukio hili lina uhusiano wa moja kwa
moja na mgogoro unaoendelea katika Chama cha Siasa Chadema. Aidha
kabla ya tukio hili, mlalamikaji amekuwa katika hali ya hofu kutokana
na kupokea simu nyingi na ujumbe mfupi (sms) wa vitisho kutoka kwa
viongozi wa ngazi mbali mbali wa Chadema ambao anadai anawafahamu.
Pia jana ofisi ya Chadema Wilaya wa Temeke ilifungwa saa 10.00 jioni
kwa kile kilichodaiwa kuwa ni maagizo kutoka katika ngazi za juu
katika chama cha Chadema. Kutokana na tukio hili nimeunda jopo la
wapelelezi waliobobea wa fani mbali mbali wakiongozwa na Mkuu wa
Upelelezi Kanda Maalum ACP. Jaffari Mohamed ili kuwabaini na
kuwakamata watuhumiwa na kuwachulia hatua kali za kisheria. Wakati
huo huo natoa
onyo kali kuwa vitendo vya utekaji nyara pamoja na madhara
yanayofuata baada ya hapo hayavumiliki katika jamii ya Kitanzania.
Yeyote
atakayegundulika kujihusisha na matukio kama haya ajue wazi kwamba
atachukuliwa hatua kali za kisheria bila ajizi na bila kujali nafasi
yake katika jamii.
Ni vizuri kila mtu au kundi lolote lenye matatizo au mgogoro lifuate
taratibu za kisheria katika kutanzua migogoro badala ya kutumia
vitisho, nguvu au utekaji nyara kama huu.
Natoa
wito kwa mtu yeyote ambaye ni raia mwema mwenye taarifa sahihi kuhusu
tukio hili awasiliane nasi ili tusaidiane kukomesha vitendo kama hivi
visirudie tena popote nchini Tanzania.
(S.
H. KOVA – CP)
KAMISHNA WA POLISI
KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments
Post a Comment