Zinazobamba

WAKILI OKECH AREJESHA FOMU YA KUTIA NIA UBUNGE KIVULE.


Na Mwandishi Wetu.

Mwenyekiti Mstaafu wa UVCCM Wilaya ya Ilala ambaye pia ni Wakili wa Mahakama kuu Dkt. Alfred Tukiko Okech amerejesha fomu ya kutia nia kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Kivule.

Okech amerejesha fomu hiyo leo Julai 2,2025 kwa katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Chief Sylvester Yaredi,baada ya kukamilisha taratibu ya kujaza taarifa muhimu.
Aidha amesema amejiridhisha vya kutosha na kuona ana uwezo wa kuongeza wananchi wa Kivule,na kuwaletea maendeleo.

No comments