ANITA WAITARA AREJESHA FOMU YA KUTIA NIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KIVULE.
Na Mwandishi Wetu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya G & S Anita Waitara amerejesha fomu ya kutia nia kugombea Ubunge Jimbo la kivule.
Anita amerejesha fomu hiyo leo Julai 2,2025 kwa katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Chief Sylvester Yaredi baada ya kukamilisha taratibu.
Aidha Anita ambaye amejipambanua kuwa mlezi wa vikundi vya wajasiliamali Wanawake,amesema amejitosa kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge ili kuondoa changamoto za miundombinu ya Barabara ambayo siyo rafiki kwa Wananchi.
No comments
Post a Comment