VETA MTWARA YAJA NA BUNIFU YA KITI KINACHOBADILIKA KUWA SOFA,KITI NA MEZA.
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Chuo Cha Ufundi Stadi (VETA) Mkoani Mtwara wametengeza bunifu ya Kiti kinachobadilika nakuwa Sofa,Kiti na Meza.
Hayo yamesemwa Julai 4,2025 Jijini Dar es salaam na Mhandisi Elias Boniface kutoka VETA Mtwara wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwenye maonyesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yenye kauli mbiu isemayo "Fahari ya Tanzania".
"Hapa VETA Mtwara kwenye banda letu la uselemara tuna bidhaa ambazo tumezileta ambazo ni bunifu zimetokana na kazi ambazo wanafunzi wenyewe wamezifanya,moja ya bunifu ambayo tumekuja nayo ni kiti ambacho kinabadilika kuwa sofa,kiti pamoja na Meza."amesema
Nakuongeza kuwa " Yote hii ni kwajili ya kuturahisishia kuondoa matumizi yasiyo sahihi au yasiyo ya lazima ndani ya nyumba,wengi wanapokua wana anza Maisha una kuta wana vyumba vidogo kwahiyo tumewaletea sofa ambalo ni Sofa,ni Kiti pamoja na Meza,ambapo akinunua sofa hili atakua amepata Meza na Kiti."
Pia amesema VETA Mtwara imekuja na bunifu nyingine ambayo ni mashine kwa ajili ya kukata chupa,mashine hiyo imewasaidia baadhi ya watu wengi, kwasababu ni mashine inayotatua moja kwa moja matatizo yaliyopo kwenye jamii.
Amesema Badala ya Chupa iliyotumika kuitupa,wao wanaikata nakuirudisha sokoni kama glasi,nakwamba mashine hiyo inatumia umeme kukata hizo chupa,ambapo kunakuwa na glascuter,kunakua na handle pamoja na sehemu ambayo ni kufunga na kuifungua chupa(Lock)
"Inapokua inazunguka sisi tunahakikisha tumeshapima vipimo vyetu kulingana na vipimo ambavyo tunavihitaji halafu tunaigandamiza inatutengenezea mistari,baada ya hapo tunaizima tunaitoa mashine yetu tunakua na maji ya moto na maji ya baridi,tunaweka kwenye Maji ya moto ukirudisha kwenye Maji ya baridi ukiweka kwenye Maji ya moto tena inakatika yenyewe."Amesema Mhandisi Boniface.
No comments
Post a Comment