MWENYEKITI TUGHE AREJESHA FOMU ZA KUTIA NIA KUGOMBEA UBUNGE KIVULE.
Na Mwandishi Wetu.
Mwenyekiti wa Chama Cha wafanyakazi wa Serikali kuu Mkoa wa Dar es salaam na Mjumbe kamati kuu (TUGHE) Brendan Maro amerejesha fomu ya kutia nia kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Kivule.
Maro ambaye pia ni Afisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) Makao Makuu Dododoma,amerudisha fomu hiyo leo Julai 2,2025 kwa katibu CCM Wilaya ya Ilala Chief Sylvester Yaredi.

Aidha amesema wakati uliyopo kwa sasa yeye anatosha kupewa ridhaa ya kuongoza Jimbo hilo kwa miaka mitano ijayo ili kumsaidia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwaletea maendeleo wananchi wa Kivule.
No comments
Post a Comment