KATIBU UWT ILALA AMEWASIHI WANAWAKE KUJITOKEZA KWA WINGI KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI
Katibu wa Umoja wa Wanawake(UWT) Wilaya ya Ilala Rosemary Mwakisalu ameomba Wanawake Wilayani humo kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kugombea Ubunge na Udiwani.
Mwakisalu ametoa wito huo leo Julai 1,2025 wakati akizungumza na Waandishi wa habari kufuatia mwenendo wa zoezi la uchukuaji wa fomu za kugombea nafasi za uongozi ndani ya chama hicho.
"Natoa wito kwa Wanawake wote wa Ilala, wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu,na gharama yetu ya fomu ni shilingi elfu 50 tu hakuna mchango mwingine wowote unaotolewa"amesema Rosemary
Nakuongeza kuwa "kwa kazi kubwa aliyoifanya Dkt Samia Suluhu Hassan,akiwa Mwanamke aliyetuonyesha njia,tuna kila sababu ya kutoka Wanawake kugombea nafasi za uongozi,usijiogope kwasabubu huna fedha,usijiogope kwasabubu ni masikini,usiogope kwasabubu huna mtu wa kukusemea.
Aidha amesema kwamba tngu kuanza kwa zoezi la uchukuaji wa fomu Juni 28,2025 ,Wanawake wanaendelea kujitokeza kwa wingi katika Wilaya hiyo kuchukua fomu kwa nafasi mbalimbali.
"Mpaka jana Juni 30,2025, jumla ya wanawake wapatao 63 walikua wamechukua fomu kugombea nafasi ya Udiwani Viti maalumu Wilaya ya Ilala,nafasi za kata Wanawake wapatao 52 walikua wameshajitokeza kuchukua fomu kugombea Udiwani wa kata."amesema
Nakuongezakuwa " Kwa nafasi ya Ubunge wa Majimbo mpaka jana Juni 30,2025 Wanawake wapatao 10 wamejitokeza kuomba nafasi ya Ubunge wa Majimbo,hivyo niwashukuru sana Wanawake waliojitokeza kuomba nafasi hizi.
Halikadhalika ameendelea kuwasihi Wanawake wengine kujitokeza kwani bado nafasi ipo,muda bado upo,ambapo mwisho wa kuchukua fomu hizo ni kesho Julai 2,2025 saa 10 kamili jioni.
Amesema Chama Cha Mapinduzi kinambeba kila mwanachama,kila Mwananchi ambaye ameridhia ndani ya nafsi yake kuomba nafasi ya uongozi.
"Bado nawasihi Wanawake,hitaji langu mimi kama Katibu wa UWT Wilaya ya Ilala,idadi bado haijaniridhisha,mpaka sasa idadi ya Wanawake waliojitokeza ni 115 Udiwani wa kata na Udiwani wa Viti maalumu,natamani nifikishe Wanawake 200."
Nakuongeza kwamba," Ngazi ya kata Wanawake wagombee,watumishi wasiogope,Mwanamke yeyote hata kama ni mama lishe,watu wenye uhitaji maalumu wajitokeze waje wachukue fomu hii fursa niya kwao,kwani nikipata watu wenye ulemavu itatusaidia kwasababu wao watakua na sauti ya kuwasemea watu wenye uhitaji watakapokua kwenye Halmashauri.
No comments
Post a Comment