TCRA YAWAONYA WANAOSAMBAZA PICHA ZA MAREHEMU,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA) imewataka
watanzania kuacha tabia ya kuweka picha mitandaoni za watu waliokufa au picha
za ngonokwa kuwa vitendo hivyo ni kosa la
jinai.
Pia Mamlaka hiyo imetaka jamii kutumia mitandao ya
kijamii kama njia bora ya kujiletea maendeleo .
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na
Mkurugenzi mkuu wa (TCRA) Mhandisi James Kilaba wakati wa ufunguzi wa semnina
ya kutoa elimu kwa viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam ili waweze kutumia
mitandao ya kijamii kwa manufaa ya nchi.
Mhandisi Kalaba amesema kwa sasa watu wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii
kwa kuweka picha ambazo hasistahili kwa
jamii.
“Leo kwa mfano ikitokea ajali ambao watu wamekufa au
kupata ajali unakuta mtu anachukua picha
hizo na kuziweka kwenye mitandao ,nataka kuwambia hili ni kosa la jinai”amesema
Mhandisi Kalaba.
Amesema kwa sasa jamii haina budi kubadilika na
kuanza kutumia mitandao kama njia ya kujiletea kipato .
“Jamii inatakiwa kutumia mitandao ya kijamii kama
njia ya kujiletea kipato,kwa mfano kwa sasa tumeanzisha anauni za makazi ambazo
hizi zitaisadia serikali kuwafahamu na kuweza kurahisisha mipango ya
kimaendeleo’amesema Mhandisi huyo.