VITA YA UCHUMI TANZANIA: LHRC YAIPONGEZA SERIKALI…YATOA UKUMBUSHO
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Bi. Anna Henga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari, kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Kituo hicho, Bw. Ezekiel Massanja. |
KITUO
CHA SHERIA na haki za binadamu (LHRC) kimepongeza juhudi zinazochukuliwa na
serikali ya awamu ya tano kwa kupambana na mafisadi, ikiwamo hatua ya kuundwa
kwa kamati mbili za Rais zilizokuwa na lengo la kuchunguza thamani halisi ya madini yaliyomo
katika makasha ya mchanga wa madini (makinikia) na ile ya kuwafikisha viongozi
waandamizi wa kampuni ya IPTL mbele ya vyombo vya sharia.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Bi.
Anna Henga amesema wamekuwa wakifuatilia kwa karibu hatua za serikali ya awamu
ya tano hususani katika suala zima la uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali za
Nchi, na kusema wamebaini kuwa serikali inapaswa kuungwa mkono ili vita hiyo ya
uchumi iweze kufanikiwa.
Amesema
ukiangalia maamuzi makubwa yanayochukuliwa na Mh. Rais yote yamelenga kurudisha
hadhi ya Taifa ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi walio wengi hivyo kuna
kila sababu ya kuumunga mkono ikiwemo kutoa ushauri mbalimbali.
“Ikumbukwe
mnamo Juni 9 mwaka 2017 kituo cha sharia na haki za binadamu kilitoa tamko hapa
mbele yenu kupinga kusudio la mamlaka ya udhibiti wa nishati na madini (EWURA)
kuiongezea muda wa kuzalisha umeme kampuni ya Independent Power Tanzania
Limited (IPTL) kwa muda wa miezi 55” na kuanzia hapo tulishuhudia hatua ambazo
zilichkuliwa na serikali kama kituo tunapongeza hatua iliyochukuliwa ya
kuwapeleka mahakamani wahusika wakuu wa kashfa ya Tegeta Escrow ambao ni zao la
kampuni ya IPTL.
Amesema
hatua zinazochukuliwa sio tu zinaleta heshima katika Taifa lakini pia
zinarejesha Imani ya Watanzania kwa serikali yao kwani wanaona kumbe dhana ya
uwazi na uwajibikaji inawezekana na pia inafuta dhana ambayo imejengeka kuwa
viongozi wanalindana.
Licha
ya kuwepo kwa pongezi hizo lakini kituo cha sharia pia kimetoa angalizo kama
kweli tunahitaji kuwa na vita ya uchumi yenye mafanikio katika Taifa la
Tanzania lazima yafuatayo yakafanyika.
…YAKUMBUSHA
YAFUATAYO KUFANYIKA
Kuundwa kwa mamlaka kamili ya madini;
Kituo
cha sharia na haki za binadamu kimeishauri serikali kuunda Mamlka kamili ya
Madini itakayokuwa inafanya kazi ya uratibu wa shughuli zote za madini Tanzania
kama zilivyo Mamlaka ya hifadhi ya Jamii. Mamlaka ambayo itakuwa na dhima ya
kushughulika na mikataba yote ya madini, mapato ya madini, kuidhinisha leseni (vibali),
kuratibu soko la madini ambapo madini yote yatauzwa hapa Nchini ili kupata
fedha za kigeni.
Waliotajwa katika kamati zote mbili
kuchukuliwa hatua, Pia kituo kimeshauri kuwa wale wote
waliotajwa katika ripote zote mbili za Rais wachukuliwe hatua ikiwamo
kuwafikisha katika vyombo vya sharia kujibu tuhuma zao.
Waitaka bunge kubadilika Kituo
cha sharia kimetaka Bunge kubadilika kwenda sambamba na kasi ya Serikali ya
awamu ya tano, lisiendeshe mijadala kisiasa bali kwa lugha za kibunge na
kutanguliza maslahi ya Nchi mbele.
“Tumefika
hapa na kashfa hizi ambazo zimedumu kwa miongo kadhaa kwa sababu ya kuwa na
bunge dhaifu lisiloweza kuisimamia serikali kwa dhati hususani katika mambo
makubwa ya kitaifa. Sasa kila hoja inayowasilisha katika bunge ipewe uzito
unaostahili pasipo kujali itikadi ya vyama ambazo kwa kiasi kikubwa imechangia
kwa kashfa hizi kuendelea kudumu kwa miongo kadhaa” Alisema.
Mambo
mengine ni pamoja na kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo, serikali kuheshimu
misingi ya haki za binadamu, serikali kuheshimu na kulinda demokrasia pamoja na
serikali kuwachukulia hatua watu wote waliohusika katika miamala ya Tegeta
Escrow. Pia imeitaka serikali kuchukua hatua katika kashfa zingine ambazo
zimesababisha Serikali kupata hasara ikiwamo kashfa ya ununuzi wa rada, kashfa
inayohusishwa na Kampuni ya Lugumi, kashfa ya Richmond, kashfa ya uwepo wa
harufu ya rushwa katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na mifuko ya hifadhi
ya jamii …mathalani mradi wa NSSF kigamboni pamoja na suala la Vitalu vya
uwindaji na umiliki wake