Zinazobamba

SHAWEJI AWATAHADHARISHA WANAOTUMIA RUSHWA UCHAGUZI MKUU.


                         Shaweji Mkumbula

.Asisitiza kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika.

.Asema CCM itashirikiana na TAKUKURU kuwang'amua watoa rushwa.

.Ilani ya uchaguzi ya 2020/2025 yatekelezwa kwa kiwango kikubwa.

Na Mwandishi Wetu.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Kinondoni Shaweji Mkumbula ametoa tahadhari kwa wanaowania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi mkuu kuachana na vitendo vya rushwa.

Mkumbula ametoa tahadhari hiyo leo februari 27,2025 Ofisini kwake Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika mahojiano maalumu nakubainisha kuwa rushwa inadumaza,na  inaleta wagombea ambao hawakubaliki kwenye jamii.

"Kimsingi mimi kama Mwenyekiti wa Wilaya nina kamati zangu,tumejipanga vizuri kuhakikisha tunadhibiti rushwa."amesema Mkumbula

Nakuongeza kwamba "Tutakutana na viongozi wenzetu wa Chama ambao ni wafanya maamuzi, kwasababu maamuzi hatufanyi peke yetu,wanafanya watu wengi kwa ajili ya kuwachukulia hatua kali wagombea wote wanohusika na vitendo vya rushwa."

Aidha amesema kuwa wamekua wakijitahidi kuhakikisha wanazuia  mianya ya rushwa,nakwamba kwenye Wilaya ya Kinondoni hawatapendekeza mgombea ambaye ni mtoa rushwa.
"Mgombea mtoa rushwa kwenye ngazi yetu sisi hatutampitisha ,,na tutasema kwanini hatumpendekezi,tunawafuatilia na tunawajua nani anatoa rushwa na nani hatoi."amesema 

Nakusisitiza kuwa,"tutazungumza pia na wenzetu wa TAKUKURU watusaidie kuwang'amua watoa rushwa,sababu mgombea akipita kwa rushwa manake kazi anayoenda kufanya sio ya Wananchi bali atafanya kazi ya kurudisha pesa zake kwasababu ametoa nyingi kwa rushwa".

Ameongeza kuwa wakati mwingine  mgombea mtoa rushwa anakua  hakubaliki kwa wananchi, hivyo moja ya kazi yao kama viongozi wa CCM Wilaya ni kuhakikisha wanapitisha mgombea anaekubalika kwa Wananchi.

Aidha amesema kuwa yeye( Shaweji Mkumbula) na wenzake hawanunuliki,nakwamba wapo  vizuri na wataendelea kusimamia misingi na maadili ya Chama Cha Mapinduzi  kwa weledi mkubwa.

Akizungumzia kuhusu Migogoro ya viongozi ndani ya chama Shaweji amesema kwamba kwa Kinondoni hakuna mpasuko wa viongozi waliokuepo na wanaokuja.

"Makundi yanakuepo hata Kinondoni yapo,hata chama chochote lazima kiwe na makundi hasa katika kipindi hiki watu wanatafuta mamlaka,lakini tumekua tukijitahidi makundi hayo yasiharibu mshikamano wa Chama chetu" amesema 
Nakuongeza kwamba 'tumeshawaita watu wote wanaoleta vurugu na wengine tumewaonya na kuwambia waache Migogoro ndani ya chama chetu."

Amesema kuwa Kinondoni ni Wilaya inayoangaliwa sana kwasababu ya historia yake na jiografia yake,ambapo viongozi wa ngazi za juu  wote wapo Wilayani humo,hivyo hakuna Migogoro yoyote na watu waliopo ndani ya uongozi na wale wanaotia nia hawana  shida nao.

Kuhusu utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2020/205,Mkumbula amesema kwamba  imetekelezwa kwa kiwango kikubwa,hivyo kuchaguliwa au kutokuchaguliwa pia siyo tu utekelezaji wa ilani ya chama pekee bali inategemeana na mgombea anavyoishi na wapiga kura,inawezekana ameishi nao vizuri wakamchagua  au vibaya ndio maana hawajamchagua.

"CCM Wilaya ya Kinondoni kimetekeleza Ilani vizuri kwasababu sisi Ilani hatumpi mtu,Ilani ile niya chama tunawapa wale wagombea wetu sasa tekelezeni akiwemo mheshimiwa Rais."amesema

Nakusisitiza kuwa,"kwenye utekelezaji wa Ilani sisi Kinondoni hatuna shida,tumetekeleza Ilani vizuri hata sasa ukipita baadhi ya maeneo utaona Ilani inaendelea kutekelezwa."

Wito wangu tuweke maslahi mapana ya chama ili tusiwe na Migogoro,tuondoe umimi,watu wanafika mahali wanasahu miiko ya chama wanajizungumzia wao kama wao,hivyo nawaomba sana waliokuepo na wanaotarajiwa kuja wasivuruge mshikamano wa chama chetu,kugombea kusikigawe chama chetu,kugombea kusivuruge chama chetu.

Hata hivyo ameongeza kuwa kubwa zaidi wote tunafahamu Rais Wetu anafanya kazi kubwa sana na anaendelea kufanya kazi kubwa sana,na bahati nzuri sisi kwenye CCM tumeshampitisha,kazi yetu kubwa sisi wana CCM Kinondoni nikuhakikisha tunazitafuta kwa wingi kwa wivu mkubwa kura za Mh.Ris ili ashinde kwa kishindo kwenye uchaguzi wa Oktoba Mwaka huu.





Hakuna maoni