PAMBANO LA "KNOCKOUT YA MAMA" AWAMU YA TATU KUFANYIKA FEBRUARI 28,2025.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mafia Boxing Promotion Ally Zayumba(mwenye kofia) akizungumza na Waandishi wa habari( hawapo pichani) kufuatia maandalizi ya pambano la ngumi litakalofanyika feb.28 2025.wengine ni mabondia watakaoshiriki katika pambano hilo.
Na Mussa Augustine.
Taarifa hiyo imetolewa leo februari 25,2025 na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw.Ally Zayumba nakubainisha kuwa uandaaji wa mapambano hayo ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta ya Michezo Nchini.
Zayumba amesema kwamba "Mapambano haya tunaya andaa kutokana na kazi anazozifanya Dkt.Samia kwa ufanisi mkubwa sana,mama (Rais Dkt.Samia) amekua mwanamichezo namba moja,amekua msimamizi mzuri wa miradi ya Maendeleo na Taifa kwa ujumla,hivyo tunamuunga mkono kupitia pambano la "Knockout ya mama tunalolifanya kila baada ya miezi miwili au mitatu"amesema Zayumba
Rais Dkt Samia Suluhu HassnNakuongeza kuwa" ukiangalia makusanyo ya kodi yanayofanyika na fedha hizo kurudishwa kwa Wananchi kwa ajili ya maendeleo,Serikali ya Tanzania tunaona manufaa makubwa sana ya kodi,hivyo tumeanzisha hii knockout ya mama ili kumuunga mkono mheshimiwa Rais Dkt. Samia kwa yale anayoyafanya kwa Taifa letu"
Aidha Zayumba amefafanua kuwa bondia Amiri Matumla,atapanda ulingoni dhidi ya mpinzani wake kutoka Namibia Paul Amavila,nakwamba pambano hilo litakuwa na mizunguko nane.
"Hili ni pambano lake la kwanza tangu ajiunge kwenye mapambano ya kimataifa na ameahidi kufanya vizuri kwa lengo la kuanza kutengeneza rekodi nzuri katika karia yake kupitia masumbwi, amesema Zayumba.
Ameongeza kwamba siku hiyo kutakua na mapambano 11 ya utangulizi yakiongozwa na mkongwe Dullah Mbabe.
Amefafanua kwamba wa mchezo wa ngumi katika kipindi hiki cha uongozi wa Rais Dkt.Samia umekuwa na mafanikio makubwa hivyo ni vema watanzania wakaendelea kumuunga mkono.
Zayumba amesema kwamba viingilio katika pambano hilo vitakuwa ni shilingi,50,000, sh. 20000 na 10,000.
Zayumba amesema kuwa mabondia wengine watakaopanda ulingoni katika mapambano ya utangulizi ni Oscar Richard atakayezipiga na bondia kutoka Malawi.
Rashid Mtange kutoka Nacoz Camp chini ya kocha Ramadhani Uhadi 'Rama Jah' atazichapa na bondia kutoka India na wengineo.
Naye Bondia Matumla, ambaye ni mtoto wa Rashid Matumla' Snake Man' amejinasibu kufanya vizuri katika pambano hilo kutokana nakwamba amefanya maandalizi ya kutosha.
'Naomba watanzania wajitokeze kwa wingi kuja kushujudia pambano hilo ambalo litakuwa na burudani ya aina yake, amesisitiza Snake Man.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni