NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI ALEXANDER PASTORY MNYETI AZINDUA RASMI MRADI WA "THE BAHARI ACCELERATOR"
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh.Alexander Pastory Mnyeti,amezindua rasmi The BAHARI Accelerator,jukwaa linalolenga kuendeleza ubunifu na maendeleo endelevu kwa kugeuza tafiti za kisayansi kuwa fursa za kibiashara katika uchumi wa buluu wa Tanzania.
Naibu Waziri Mnyeti amezindua Mradi huo Februari 24,2025 Jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya wiki ya Bahari yanayofanyika kwa siku tano katika hotel ya Ramada Jijini humo.
Mradi huu upo chini ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwa kushirikiana na Twiga Connect Platform kama washirika wa utekelezaji na washauri wa masuala ya uwekezaji na biashara.
Aidha Mradi huo umelenga kutoa Fursa kwa Watafiti, Wajasiriamali Wawekezaji kwenye uchumi wa buluu endelevu pamoja na kubadili Sayansi kuwa biashara.
"Lengo kuu la The BAHARI Accelerator ni kuendeleza ubunifu na maendeleo endelevu kupitia biashara za kisayansi kwa kugeuza tafiti za kisayansi kuwa fursa za kibiashara katika uchumi wa buluu wa Tanzania."amesema Nakuongeza kuwa Mhe. Rais Dkt.Samia ameweka nguvu kubwa kwenye uchumi wa Buluu kwa kuanza na elimu kwa wavuvi na wananchi wetu, Elimu hii itawafanya kujua nini kilichopo kwenye uchumi wa buluu” amesema Naibu Waziri huyo wa Mifugo na Uvuvi.
Aidha ameongeza kuwa jitihada anazoendelea kufanya mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani ni utoaji wa boti za uvuvi, vizimba na kuwezesha kilimo cha zao la mwani.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa wa Taasisi ya utafiti wa uvuvi nchini (TAFIRI)Dkt. Ismael Kimirei amesema taasisi hiyo itawasaidia wavumbuzi na watafiti kwa kuyachukua matokeo yanutafiti na kuyawekea msingi ili yawe na tija iliyokusudiwa.
Maadhimisho ya wiki ya bahari yanafanyika katika Hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam kwa muda wa siku tano kuanzia leo Februari 24 hadi 27 mwaka 2025 na yanahusisha wadau kutoka mataifa mbalimbali Duniani.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni