Zinazobamba

RC CHALAMILA KARIAKOO KUANZA BIASHARA SAA 24

-Asema Mataifa yaliyoendelea kote Duniani hufanya biashara usiku na mchana.

-Asistiza DSM kitovu cha biashara lazima biashara ifanyike saa 24, 

-Awahakikishia wafanyabiashara usalama wa kutosha.

-Asema baada ya uzinduzi ataunda kamati itakayoongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa kupitia Sheria zinazokinzana na biashara saa 24.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo leo Februari 24,2025 kwa nyakati tofauti akiwa katika Studio za Crown Media na Kariakoo akiwa anaongea na waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali. 

RC Chalamila amesema kwa siku tatu mfululizo kuanzia Februari 25,2025 mpaka kilele chake  Februari 27,2025 tunautangazia umma kuanza rasmi kwa biashara saa 24 ambapo Kariakoo ni eneo la uzinduzi lakini wilaya nazo zitaendelea kufanya hivyo Katika maeneo yao ili kuweza kurasimisha biashara saa 24.

Aidha RC Chalamila amesema Mataifa yaliyoendelea hufanya biashara saa 24 ambayo hupanua wigo wa ajira kwa vijana, lakini pia kuongezeka kwa kodi hivyo kwa kuwa Mkoa huu ni kitovu cha Biashara kwa kufanya hivyo vijana watapata fursa za kujiajiri na TRA pia itaweza kukusanya mapato mengi zaidi.Sambamba na hilo RC Chalamila amewahakikishia wafanyabiashara usalama wa kutosha wasiwe na shaka Dar es Salaam ni salama sana miundombinu ya kiusalama inaendelea kuimarishwa ikiwemo kuwekwa taa na Camera katika Mitaa.

Vilevile RC Chalamila amesema baada ya uzinduzi huo anatarajia kuunda kamati itakayoongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila kwa ajiri ya kupitia sheria zinazokinzana na kufanya biashara saa 24 hasa Sheria ndogo ndogo za Halmashauri za Manispaa. 

Wananchi wamepongeza uamuzi wa Serikali kufanya biashara saa 24 kwa kuwa unafaida kubwa kiuchumi.

Hakuna maoni