RAIS MWINYI: UMOJA WA ULAYA UNA MCHANGO MKUBWA ZNZ
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amefahamisha kuwa Umoja wa Ulaya una Mchango Mkubwa na Muhimu kwa Maendeleo na Sekta ya Uwekezaji pamoja na ustawi wa maisha ya Wananchi.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipofungua Kongamano la Biashara la Zanzibar na Umoja wa Ulaya , Hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa Ndege ,Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameuhakikishia Umoja wa Ulaya kuwa Serikali inachukua Juhudi maalum Kuandaa Mazingira mazuri ya Uwekezaji hapa nchini ili Wawekezaji wanaokuja wawekeze katika Mazingira Bora na endelevu.Halikadhalika, Rais Dkt. Mwinyi amesema Zanzibar itaendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya katika nyanja mbalimbali za Maendeleo kwani ni mshirika Muhimu katika Juhudi za kukuza Uchumi.
Amebainisha kuwa Uwekezaji wa Umoja wa Ulaya hapa Zanzibar unachangia Asilimia 31 ya Miradi yote ya Uwekezaji iliosajiliwa unaofikia thamani ya Euro Bilioni 2.8 na kutoa fursa za Ajira Elfu 19.
Rais Dkt.Mwinyi alishuhudia Utiaji Saini wa Mkataba wa Ushirikiano Baina ya Umoja wa Ulaya na Mamlaka ya Uwekezaji ya Zanzibar (ZIPA) pamoja na kuzindua Ripoti ya Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya hapa Zanzibar ya Mwaka 2023.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni