Zinazobamba

MWENYEKITI NEC AAHIDI UADILIFU KAZINI...


jaji-kaijage-1DAR ES SALAAM: MWENYEKITI mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Semistocles Kaijage,  anayeshika nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mstaafu Damiani Lubuva aliyemaliza muda wake Desemba 19 mwaka huu amesema kuwa katika msingi wa uongozi wake anategemea kutenda haki kwa kuzingatia sheria na taratibu za kiapo alichoapishwa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli.
jaji-kaijage-2Ameyasema leo wakati alipoulizwa swali na mwandishi wa habari katika ofisi za NEC jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa juu ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa ubunge na madiwani utakaofanyika Januari 22,2017.
jaji-kaijage-3AlisemaTume ya Taifa ya Uchaguzi kwamujibu wa kifungu cha 37 (1)b cha sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura ya 343 ilitangaza kufanyika kwa uteuzi wa wagombea wa uchaguzi huo Desemba 22 mwaka huu ambapo  jumla ya vyama vyenye wagombea kwa jimbo la Dimani, Zanzibar, ni 11 na wote wakiwa ni wanaume.
Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ofisini kwake leo.
“Kwa upande wa udiwani, katika halimashauri 20 za Tanzania bara, vyama vyenye wagombea ni 13. Jumla ya wagombea wa nafasi ya udiwani ni 72 na kati ya wagombea hao wanawake ni watano na wanaume 67.
Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ofisini kwake leo.
“Hadi sasa pingamizi zilizokatwa ni sita, ambapo tano zimekatwa kwenye kata ya Ihumwa Manispaa ya Dodoma na moja katika kata  ya Isagehe Halmashauri ya Mji wa Kahama.
 Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kulia) akiwa Ofisini kwake kwa mara ya kwanza mara baada ya kuapishwa leo. Mhe. Jaji Semistocles Kaijage ameteuliwa kuongoza Tume hiyo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia tarehe 20 Desemba, 2016.
Aidha alifafanua kuwa kwa mujibu wa ratiba  ya uchaguzi tayari kampeni zimekwaishaanza leo na zinategemea kufikia mwisho Januari 21,2017 na kamati za maadili zinaendelea kuundwa katika ngazi mbalimbali ambapo zitakuwa na jukumu la kusimamia utekelezaji wa maadili katika kipindi chote cha kampeni.
Baadhi ya Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakimpokea Mwenyekiti mpya wa Tume hiyo mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Posta, jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakimpokea Mwenyekiti mpya wa Tume hiyo mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Posta, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan (kushoto) akimkaribisha Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kulia) kwenye Ofisi za Tume zilizoko Posta jijini Dar es salaam. Mhe. Jaji Semistocles Kaijage ameapishwa leo Ikulu jijini  Dar es salaam kuiongoza Tume hiyo kwa kipindi cha miaka 5.