Tanzia: Mpiga picha maarufu Mpoki Bukuku afariki dunia kwa ajali
Dar es Salaam; Tasnia ya habari imepata pigo kubwa kufuatia mpiga picha maarufu hapa nchini, Mpoki Bukuku aliyefariki dunia leo katika Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kwa Umma (MOI) Almas Jumaa.
“Ni kweli Mpoki amefariki dunia
mchana huu, alipokelewa jana usiku baada ya kupata ajali ya gari maeneo
la Mwenge ITV, taarifa zaidi tutazitoa baadaye,” alisema Almas.
Mpoki Bukuku amewahi kufanya kazi kama Mpiga Picha Mkuu katika gazeti la Mwananchi, Majira na Nipashe.