MBUNGE WA UKAWA AMBWAGA MAGUFULI NA SERIKALI YAKE MAHAKAMANI,BOMOABOMOA YASITISHWA RASMI,ZITTO KABWE AMVULIA KOFIA MBUNGE MTULYA,SOMA HAPO KUJUA
Wakazi wa mabondeni wakishangilia nje ya mahakama baada ya Mahakama ya Ardhi kutangaza kusitisha bomoabomoa |
Mahakama ya Kuu
ya Ardhi imetoa amri ya kusitisha zoezi hilo la kubomoa hadi kesi ya msingi
iliyofunguliwa mahakamani hapo itakaposikilizwa.
Ombi hilo lilitokana na malalamiko ya wakazi wengi walioiomba
mahakama izuie bomoabomoa hiyo kutokana na madai ya ukiukwaji wa haki zao
ambapo wengi wa walalamikaji hao walidai kufidiwa kabla ya kuondoka.
Hata hivyo uamuzi huo wa mahakama umewagusa walalamikaji 674 tu
ambao wametajwa kwenye malalamiko huku zoezi la bomoabomoa likiendelea kama
kawaida kwa nyumba zingine ambazo hazihusiki na kesi hiyo.
WAKATI mahakama
kuu ikisimamisha zoezi la bomoa bomoa, Mkuu wa Mkoa Dar eS Salaam, Said
MeckSadick amejiteteana kukanusha taarifa za upotoshaji ambazo zimekuwa
zikitolewa na viongozi wa kisiasa hususani wenyekiti wa mitaa na baadhi ya
wakazi wanaoishi maeneo hatarishi ya mabondeni juu ya serikali
kuvunja nyumba, ikizingatia kutotoa maeneo mbadala ya kujenga makazi mapya
ya kudumu. Anaandika Aisha Amran ….
(endelea).
Mecksadick amesema mwaka 2011 yalipotokea
mafuriko serikali iliwapatia viwanja wakazi waliokuwa na
nyumba katika maeneo hatarishi ya mabondeni kwa
Wilaya zote tatu za Mkoa Dar es Salaam katika eneo la Mabwepande
wilaya Kinondoni.
Kwa mujibu mkuu wa mkoa jumla ya viwanja 1007 viligawiwa kwa
wakazi hao wa mabondeni na viwanja vitatu havigukawiwa kwa sababu
viliangukia maeneo yasiyofaa kwa makazi.
Aidha sambamba na kupatiwa viwanja wakazi hao walipatiwa
misaada ya kibinadamu pamoja na vifaa vya kiujenzi ikiwemo mifuko ya
saruji 100 mabati na mbao kila kaya na kuwawekea huduma muhimu
za kijamii.
Amesema wakazi hao wamediriki kuuza viwanja vyao kwa bei ya
chini na kurudi maeneo waliokuwa wakiishi awali na wengine kuuza na
kupangisha nyumba zao walizojenga mabondeni licha ya Serikali
kuwataka waondoke katika maeneo hayo hatarishi.
Vile vile amesema Serikali kwa kushirikiana na halmashauri zote
nchini imeanza na inaendelea na zoezi la bomoa bomoa kwa ajili ya kuwaondoa
wakazi wote wanaoishi maeneo hatarishi na wale waliovamia
maeneo yasiyostahili kujengwa.
Pia amesema zoezi hili la bomoa bomoa litafanyika nchi
nzima ambapo kwa sasa limeanzia Mkoa Dar es Salaam na
wakazi waliojenga katika maeneo hatarishi wabomoe wenyewe na
kuondosha baadhi ya vifaa vya ujenzi ambavyo
vitawasaidia kwenda kuendeleza makazi mapya katika viwanja
walivyopewa na serikali.
Amewataka wananchi kuacha kuendelea kulalamika wakati
wanafahamu kuwa wamevunja sheria licha ya serikali kuwataka kuondoka
kabla hawajapata madhara ikiwemo kuvunjiwa nyumba zao.
ZITTO KABWE NAYE ANENA
"Ndg. Mtulya, Mbunge Kinondoni (CUF) umeweka msingi wa kutetea wananchi
wako. Hongera sana kwa hatua muhimu sana ya leo ambayo imeonyesha uwepo wa
utawala wa sheria nchini kwetu."-Zitto Kabwe
Hakuna maoni
Chapisha Maoni