WAZIRI MWAKYEMBE AING'ANG'ANIA KATIBA YA SITTA,AIBUKA NA KUSEMA KIPORO CHAKE LAZIMA KIMALIZIWE,SOMA HAPO KUJUA

WAZIRI wa Katiba na sheria,Dk Harrison Mwakyembe ni
kama ameanza kujiingiza kwenye msuguano na wanasiasa,viongozi wa dini,mara baada
kusema mchakato wa kumalizia kiporo cha Katiba mpya huko palepale.Anaandika
KAROLI VINSENT endelea nayo.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo Jijini Dar es
Salaam wakati alipofanya ziara kwenye ofisi ya Mwendesha mastaka wa serikali
nchini,DPP ambapo amesema suala la kuendelea na mchakato wa kuipigia kura
katika iliyopendekezwa na iliyokuwa Bunge maalum la Katiba ipo pale pale
kinachosubiliwa ni Rais John Magufuli kutangaza siku ya kura ya maoni.
“Jamani wote kwa pamoja mlimsikia Rais Magufuli
amesema anakiporo cha Katiba mpya,,maana yake Rais ni mkuu wanchi ameshasema na
kila mtu alimsikia kwahiyo mchakato wa kupiga kura katiba pendekezwa upo palepale”amesema Waziri
Mwakyembe.
Kauli hii ya Mwakyembe juu ya uwepo wa kuendelea na
mchakato wa katiba mpya unaweza kuibua majadala mkubwa na kuleta
sintofahamu,kwani kipindi kile wakati lilokuwa Bunge maalum la Katiba
lilivyokuwa linatunga Katiba Pendekezwa kuliibuka msuguano mkubwa kati ya
serikali na viongozi wa dini na wanasiasa.
Wote kwa pamoja wanasiasa na viongozi wa dini
waliitoa matamko na kudai hawaitaiuunga mkono Katiba pendekezwa kwa madai
imeshindwa kuendana na maoni ya wananchi yaliyotokana na iliyokuwa tume ya ukusanyaji
maoni ya kwenye Katiba mpya,iliyongozwa Jaji Warioba.
Katika hatua Nyengine Waziri Mwakyembe ametoa
masikitiko yake kwa kudai wizara ambazo anaziona zitamwangusha Rais Magufuli ni
wizara ya Katiba na sheria ambayo inayoiongoza pamoja na Wizara ya Mambo ya ndani
ya nchi inayoongozwa na Waziri Chalres Kitwanga kwa madai ndizo zinakithili kwa
rushwa.
“Hizi wizara kusema kweli zinanuka rushwa azitendi
haki zimekuwa zinawabambikia watu kesi kwa makusudi kwa kisingizio cha kutaka
pesa,na wakiendelea hivi lazima kasi ya Rais Magufuli itapunguzwa na watu hawa”amesema
Mwakyembe.
Waziri Mwakyembe amebainisha kuwa hata kubali kuona
kasi ya Rais Magufuli inaangusha na watu wa wizara yake kwani amedai kuwafukuza
kazi watumishi ambao atawabaini wanapokea rushwa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni