KATA YA SARANGA WAPANDA MITI KUUNGA MKONO KUMBUKIZI YA SIKU YA KUZALIWA RAIS.DKT SAMIA SULUHU HASSAN.
Diwani wa kata ya Saranga Eng.Jonh Sangapi(aliyebeba mti) akipanda mti katika eneo la Zahanati ya Saranga ikiwa ni kunga mkono kumbukumbu ya Kuzaliwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Na Mussa Augustine.
Wananchi wa Kata ya Saranga, wakiongozwa na Diwani wa kata hiyo,Mh.Eng.John Sanga,wamepanda miti katika maeneo mbalimbali ya kata hiyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agenda ya 27 ya Kijani iliyoasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza leo Januari 28,2026 na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mara baada ya zoezi hilo,Diwani Sanga amesema kuwa wananchi wa kata ya Saranga wameamua kuungana kwa pamoja kama ishara ya kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.
Diwani huyo ameongeza kuwa jumla ya miti takribani 430 ya matunda na kivuli imepandwa katika maeneo mbalimbali,hususan katika shule za Msingi,shule za Sekondari pamoja na Zahanati,ikiwa ni hatua ya kulinda mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
“Sisi kama Serikali ya Kata ya Saranga tunamtakia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan heri ya siku ya kuzaliwa kwake kwani ni kiongozi anayejitoa kuwatumikia wananchi na tuna imani kubwa na uongozi wake,” amesema Eng.Sanga.
Hata hivyo amewataka Wananchi wa kata ya Saranga kutambua kuwa ni wajibu wao kuitunza miti iliyopandwa na kuhakikisha inahifadhiwa vizuri ili iweze kutengeneza unyevunyevu utakaosaidia kupunguza athari za ukame katika kata hiyo.
Kwa upande wake Afisa kilimo wa kata hiyo Bi Julieth Joshua Loi amewashauri Wananchi kuitunza miti iliyopandwa katika eneo la Zahanati ili iweze kuwasaidia wagonjwa wanaoenda kutibiwa waweze kupata kivuli na matunda kama sehemu ya lishe bora pamoja na kuhifadhi Mazingira.
Nae Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Saranga Halifa Abdalah Mdani amewashukuru Wananchi wa Mtaa huo kwa mwitikio wao mkubwa wa kujitokeza kupanda miti hiyo nakwamba viongozi wa mtaa huo wataendelea kusimamia miti hiyo ili iweze kukua.
Halikadhalika Mwenyekiti wa Baraza la usuluhishi la kata hiyo Mzee Juma Mtima,amewaasa Wananchi wa kata hiyo wawe na utamaduni wa kupanda miti katika maeneo ya Mazingira wanayoishi ili wapate hewa safi,pamoja na kuhifadhi Mazingira.
~2.jpg)











No comments
Post a Comment