Zinazobamba

ENG.SANGA AZUNGUMZIA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO NDANI YA SIKU 100 ZA DKT SAMIA MADARAKANI.

Na Mussa Augustine.

Kata ya Saranga iliyopo Manispaa ya Ubungo,imetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Sekta ya Afya, Elimu,Maji,Miundombinu ya barabara,ndani ya siku miamoja ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani.

Hayo yamesemwa leo Januari 28,2026 na Diwani wa Kata hiyo Mh.Eng.Jonh Sanga wakati akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake nakutumia fursa hiyo kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza ahadi zake kwa vitendo. 

*Sekta ya Afya.

Akizungumzia Sekta ya Afya Diwani huyo amesema kuwa Serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya kujenga Zahanati itakayo hudumia Wananchi wa kata kata hiyo hususani Wananchi wa Mtaa wa Saranga na Ukombozi. 

"Imekua kilio kikubwa kwa Wananchi wangu kukosa huduma za Afya,lakini Serikali imetimiza wajibu wake na kituo kipo mbioni kufunguliwa kwa ajili ya kuhudumia Wananchi,eneo lililobaki ni eneo la kuchomea taka pekee,lakini miundombinu mingine yote ya Zahanati imekamilika kama vile maabara,wodi za kupimia watoto na mama wajawazito pamoja na vyoo." amesema 

*Sekta ya Maji.

Aidha amesema kuwa Rais Dkt Samia pia ametoa shilingi milioni 380 kwa ajili ya mradi wa Maji wa ujulikanao *King'ong'o Water boosting*ambapo maeneo ambayo yalikua na changamoto kubwa ya maji katika Kata ya Saranga ni mtaa wa King'ong'o,hivyo kwa sasa asilimia zaidi ya 70 ya Wananchi wa Mtaa huo wanapata huduma ya Maji safi na salama.

"Isipokua kwa yale maeneo madogomadogo kulingana na hali ya mgao uliokuepo na maeneo mengi yenye muinuko bado yana changamoto ndogondogo ambayo tunaimani na Serikali itatatua changamoto hiyo kwenye maeneo hayo."amesema Eng.Sanga.

Aidha amesema kuwa hivi karibuni Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alimtuma Waziri wa Maji Jumaa Aweso katika mtaa wa Ukombozi kwa ajili ya kuangalia changamoto ya takribani miaka sita ya ukosefu wa maji katika mtaa huo ambapo alitoa maelekezo ya mradi huo kukamilika haraka iwezekanavyo.

"Huu mradi upo kwenye mchakato wa manunuzi,maana yake tayari tenda imeshatangazwa na mkandarasi amepatikana kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo wa bomba la nchi kumi na mbili"amesema.
*Miundombinu ya Barabara.

Kuhusu miundombinu ya Barabaraa amesema kuwa Rais Dkt Samia ametoa fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Morogoro ambayo inapanuliwa zaidi kutoka kwenye njia nne mpaka njia sita,lakini pia kutakua na michepuko miwili,hivyo kutakua na njia nane,mradi huo unanufaisha moja kwa moja Wananchi wa kata ya Saranga kwasababu kituo kikubwa cha mabasi ya  mwendokasi cha Kimara mwisho kipo ndani ya kata hiyo".

Amesema kuwa kata hiyo pia inatarajia kunufaika na mradi wa barabara ya Suka-Golani ambayo inajengwa kwa kiwango cha changarawe ili kuondoa changamoto ya muda mrefu iliyokua ikiwakumba  Wananchi.

" Ule mradi upo chini ya DMDP ambapo inatakiwa ijengwe kwa kiwango cha zege,lakini kwa sasa wakati bado upembuzi yakinifu naendelea,Serikali imeweza kutoa fedha ya kukarabati ile barabara na mkandarasi yupo eneo la mradi (site)anamwaga vifusi ili asambaze"amesema 

Nakuongeza"Barabara ya Temboni kuelekea Zahanati ya Saranga,tayari ina mkandarasi ambaye anatakiwa aichonge kwa kiwango cha changarawe ili Wananchi waweze kupita,na hata jana(Januari 27)nimefanya ziara na watalaamu wa Wakala wa barabara Mijini na Vijijini (TARURA) ili kuona tuanze na maeneo gani korofi ili tumalize ukarabati huo kwa muda uliopangwa" 

*Mikopo ya asilimia 10.

Amesema kuwa Rais Dkt Samia ametoa maelekezo ya uanzishwaji wa majukwaa ya Wanawake kwa ajili ya mikopo ya asilimia 10,ambayo inalenga Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu,ambapo tayari majukwaa hayo yameshaanzishwa kwa ajili ya wanufaika wa mikopo hiyo waanze kunufaika.

*Ulinzi na Usalama.

Akizungumzia kuhusu Ulinzi shirikishi Diwan huyo amesema kuwa wakati akiingia madarakani amekuta baadhi ya maeneo katani humo yana changamoto ya ulinzi na usalama kwa Wananchi kutokana na vituo viwili vya polisi kuchomwa moto kufuatia maandamano ya Oktoba 29,2025.

" Nilianza kutengeneza Ulinzi shirikishi,kata ya Saranga ina mitaa tisa(9) ya kiserikali,lakini nina takribani vikundi thelathini na sita(36) kwa ajili ya ulinzi shirikishi,kazi kubwa ni kusimamia usalama wa Wananchi mchana na usiku." amesema 

Nakusisitiza kuwa"tunatarajia  kujenga kituo cha polisi kwenye mtaa wa Saranga na Ukombozi,Wananchi tumeshikamana kufanya hivyo ili kupunguza matendo ya uhalifu,na mimi kama msimamizi mkuu niliechaguliwa na Wananchi kwenye kata hii nitahakikisha sitamuangusha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan." 

*Sekta ya Elimu.

Kuhusu Sekta ya Elimu amesema kuwa kata hiyo ina shule sita za msingi,pamoja na shule tatu za Sekondari, nakubainisha kuwa wanafunzi wengi wamehamia kwenye kata hiyo,nakwamba wanafunzi takribani asilimia 75 wamekwisha kuripoti shuleni,ambapo hadi kufikia Februari 15 asilimia 25 ya  wanafunzi waliobaki watakua wamesharipoti nakuendelea na masomo.

Diwani huyo amehitimisha kwa kusema kuwa kata ya Saranga inakumbwa na changamoto ya Miundombinu ya barabara na vivuko,nakwamba hivi karibuni amepata makaravati 15 ,nakuyagawa kwenye maeneo korofi kwa ajili ya kutengeneza vivuko ambavyo wanafunzi na Wananchi kwa ujumla wanatumia kuvuka.





No comments