Zinazobamba

CCM: Atakaepandikiza Ukabila, Udini na Ubaguzi asiachwe atambe


Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi   kusisitiza kwakuwa Sheria  halali za nchi  zipo, zitamkabili mtu yoyote  , kikundi na watu wenye  ndoto za kufanya ushawishi wa    kupandikiza Siasa za Ubaguzi, Ukabila na Udini.

Katibu  wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar Idara ya Itikadi , Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto  Khamis, ameeleza hayo huku akisema mikono  ya sheria ianze kuwatia mbaroni wale  wote wenye kusudio hilo .

Mbeto  alisema  Sheria  ni msumeno hivyo  mtu au watu wanaofikiri wanaweza kufanikisha mradi hatari  wa kuwagawa wananchi , waangukiwe  na mkono wa Sheria.

Alisema kwa uzoefu utokanao na hatari iliozikumba  nchi kadhaa kutokana na uchochezi wa  ukabila ,ubaguzi na  udini , na matokeo  yake  yameleta madhara na maafa  hivyo yasiachwe yachipue, yakue  na kustawi .

"Kuna  baadhi  ya Wanasiasa  aidha kutokana na kufilisika kwao  kisiasa, wakianza kutumia   lugha  za Ubaguzi, Udini na Ukabila wadhibitiwe  . Sheria zipo   hivyo  zisimwache mtu atambe mitaani "Alisema  Mbeto .

Katibu huyo  Mwenezi alisema kuna maadui watatu   Ujinga , Umasikini na Maradhi,  lakini pia  maadui wa  usalama wa Taifa na Amani yetu  ni  Udini, Ukabila na Ubaguzi. 

"Vyama vyote vya Siasa vina sera zake. Program za kisiasa na kioganaizesheni. Ikiwa vipo  vyama havina  sera viache Siasa .Kutumia ukabila, udini na Ubaguzi katika Siasa ni kwenda kinyume  na Sheria "Alieleza 

Aidha, Katibu Mwenezi   huyo alisema Sheria ya Usajili wa Vyama Vya Siasa  Namba  5 ya Mwaka 1992, inakataza matumizi ya siasa za Ubaguzi, Udini na Ukabila katika Uwanja wa  kufanyia Siasa. 

Mbeto  aliongeza kusema   endapo sheria   zinazopiga marufuku mambo hayo hatari kwa taifa ,ikiwa zitakaa kimya ,kadri siku zinavyokwenda mbele , itaonekana masuala hayo ni mambo ya kawaida .

"Hivi sasa kuna baadhi  ya Vyama vy Siasa  Uongozi wote wa juu umeshikwa aidha na viongozi wa dini moja. Baya zaidi  ukakuta wanatoka kanda moja pia si ajabu  wakawa kabila  moja" Alisistiza Katibu  huyo.

No comments