Zinazobamba

SHEKHE PONDA AIPONDA CCM,ADAI SERIKALI YAKE HAINA JIPYA KUWAONGOZA WATANZANIA.


*Awaomba Wananchi kushiriki uchaguzi kuing'oa CCM madarakani Oktoba Mwaka huu.

Na Mwandishi Wetu.

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania na Mwanasiasa Mkongwe Shekhe Ponda Issa Ponda amewaomba Watanzania kukichagua chama Cha Act Wazalendo katika uchaguzi Mkuu utakofanyika Oktoba mwaka huu. 

Shekhe Ponda ambaye hivi karibuni amejiunga na Act Wazalendo ametoa rai hiyo leo Juni 14,2025 Jijini Dar es salaam,kwenye Mkutano wa hadhara uliyofanyika katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke ambapo amebainisha kwamba kwa sasa CCM hakina jipya katika kuwaletea maendeleo wananchi. 

Aidha amesema kwamba hali ya Maisha ya Watanzania walio wengi inazidi kuwa mbaya,huku vitendo vya utekaji na kupotea kwa Watu katika Mazingira ya kutatanisha vikizidi kuongezeka ambapo Serikali ya CCM imeshindwa kudhibiti hali hivyo. 

*Ndugu zangu Wananchi nimesimama hapa kwa kofia mbili, kofia ya kwanza ni kiongozi wa dini, naya pili ni kofia ya siasa kwani tayari nimechukua kadi ya Chama Cha Act Wazalendo ili niwe na sifa kisheria ya kusimama kama mwanasiasa kuwapigania Watanzania waliopoteza matumaini na haki zao muda mrefu" amesema Shekhe Ponda mbele ya hadhira. 

Nakuongeza kwamba"Serikali imeshindwa kudhibiti utekaji,Wananchi wanaishi katika umasikini uliokithiri,ukienda Hospitali kupata huduma gharama ni kubwa,Maiti zinadaiwa,CCM ipo madarakani kwa zaidi ya miaka 50,nawaomba mwaka huu tufanye mabadiliko,tuichague Act Wazalendo ili tuweze kuleta mawazo mapya ya kuwatatulia changamoto zenu Watanzania."
Awali akizungumza Kiongozi wa Act Wazalendo Dorothy Semu pamoja na mambo mengine amesema kwamba Vijana wa kitanzania bado wanahangaika kutafuta ajira,hivyo amewahamasisha wananchi kushiriki uchaguzi ili kwenda kuiondoa Serikali ya CCM iliyoshindwa kutimiza wajibu wake wa kumkomboa Mtanzania.

" Tumeona jinsi ambavyo wahitimu wa vyuo vya ualimu wamekua wakilia na kulalamika ,Serikali inasema kwamba walimu wapo wa kutosha lakini tunajua mahitaji ya walimu ni zaidi ya walimu laki mbili na sabini, walimu waliopo mtaani ni zaidi ya walimu laki moja na arobaini"amesema Dorothy Semu ambaye pia ni Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho.

Nakuongeza kwamba" hali hiyo ndivyo ilivyo kwenye kada nyingine zozote ikiwemo Afya na Kilimo,ambapo tumeona CCM ilivyofanya Afya ya Mtanzania kua bidhaa,leo hii Watanzania wanatibiwa kwa bima ya vifurushi tunatambua kwamba Afya sio kama shati ambalo kila mtu anaenda kununua kwa jinsi anavyoweza,tunasema hivi tunakwenda kutumia jukwaa la uchaguzi kama jukwaa la kuikataa CCM. 
Nae Makamu Mwenyekiti Act Wazalendo Isihaka Mchinjita amesema kwamba Serikali iliyoshindwa kutataua kezo za wananchi wajibu wa raia  ni kuhakikisha wanahamasishana kuiondoa madarakani,nakuiweka Serikali ambayo ni mkombozi wa Maisha yao.

"Kama Serikali itaheshimu kura basi wananchi watumie kura kuiondoa,kama Serikali itatumia vibaka kuiba kura wananchi wakatae kuibiwa kura,Serikali ya namna hiyo haisusiwi,hapo CCM walipofika leo hawawezi tena kuiongaza nchi hii,nawaomba tunapoenda kwenye uchaguzi wa Mwaka huu tuuchukilie ni ukombozi wa Taifa letu"amesema Mchinjita.
Hata hivyo Katibu Mkuu wa Chama hicho Ado Shaibu amefafanua  kwamba Mzunguko wa kumtambulisha Shekhe Ponda hautaishia Temeke pekee bali utaendelea kufanyika Ubungo,Kinondoni,Mbagala,Chamazi,pamoja na Majimbo yote ya Mkoa wa Dar es Salaam huku akiwaomba Wananchi kujitokeza kwa wingi.



No comments