Zinazobamba

KATIBU JESSICA MSHAMA AWAFUNDA MABINTI KUHUSU SAFARI YA UONGOZI


KATIBU wa Uhamasishaji na Chipukizi wa  (UVCCM), Jessica Mashama, amewafunda mabinti kuhusu safari ya uongozi, huku aliwataka kuongeza juhudi katika mapambano yao kufikia ndoto zao za uongozi.

Katibu Jessica ameyasema hayo, alipozungumza na mabinti wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, kampasi ya Mlimani alipofika kwaajili ya mafunzo.

Jessica, aliwata mabinti, kuweka nia thabiti na wajipambanue  wafanikiwe katika uongozi kwani sio njia rahisi; ni safari inayohitaji maandalizi na kujifunza kila siku watumie fursa za interneti kujifunza kutoka kwa waliowatangulia wasome, wajielimishe na wajiifunze jinsi ya kuvuka changamoto kwa ustadi na uimara.

"Jitengenezee fursa nje ya siasa, jitahidi kuwa na “side hustle” inayokuingizia kipato. Chagua Biashara au Shughuli ambayo unaweza kuifanya kwa ujasiri na bidii. Anza leo, hata kama ni kidogo, na uifanye kwa makini. Fursa hazisubiri; zipange na uzitekeleze

Aliwahimiza mabinti kuchagua marafiki wanaowachochea,marafiki wanajukumu kubwa katika mafanikio, kuchagua marafiki wanaokupa changamoto za kiakili, wanaokushauri, na wanaokuhamasisha kufikia malengo."Vijana, tupiganie ukombozi wetu wa kifikra sasa ni wakati wa vijana wa Tanzania kujitokeza na kupigania ukombozi wetu wa kifikra. 

Tuwe wabunifu, tuchangamke, na tuhakikisha tunashiriki kikamilifu katika kujenga mustakabali bora. Jitokeze kujiandikisha kama mwanachama wa CCM ikiwa bado hujafanya hivyo, na tuungane kuhakikisha tunachagua viongozi bora.

Vilevile, aliwataka kupiga kura ni haki yako ya msingi wajiitokeze kupiga kura ni haki yako ya msingi iliyolindwa na katiba kwani ni silaha yako ya kubadilisha mustakabali wa taifa, wajitokeze, piga kura, na uchague viongozi wanaostahili kuongoza.



No comments