NIPO TAYARI KUWATUMIKIA WANANCHI WA KINYEREZI: MREMA
Mgombea Udiwani wa kata ya Kinyerezi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Jonh Ryoba Mrema maarufu kama "Wahenga" amesema kwamba yupo tayari kuwatumikia wananchi wa Kata ya Kinyerezi endapo watampa ridhaa ya kuwatumikia katika uchaguzi mkuu ujao wa Oktoba,2025.
Ameyasema hayo leo Agost 15,2025 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhiwa barua ya uteuzi wa kugombea nafasi hiyo kutoka kwa katibu wa CCM Ilala Chief Sylivester Yared.
"Sisi familia yetu ni watu wa kawaida kabisa,lakini nimeaminiwa na wajumbe,Chama kimeniamini,sasa nimepata nafasi yakuenda kuomba ridhaa kwa Wananchi wa kata ya Kinyerezi ili wanichague mimi niwe diwani wao ili tuendeshe gurudumu la Maendeleo"amesema Mrema.
Nakuongeza" Nashukuru sana Mwenyekiti Wetu wa Chama ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka Mazingira sawa ya Ushindani ndani ya Chama,nitoe wito kwa watu wenye ndoto ya kutafuta uongozi kwenye Nchi yetu kama kuna mtu anaamini kwamba ili upate uongozi ndani ya chama chetu lazima lazima uwe na connection hao watu wanakudanganya hawafikirii sawa sawa"
Amesema kuwa yeye alipotokea baba yake au mama yake,au ndugu yake yeyote yule hajawahi kuwa hata Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji,hivyo yeye aliamka asubuhi akiwa na ndoto kichwani ya kuwa diwani akaenda kuchukua fomu akaijaza nakuirudisha akiamini kuwa kila mtu anayo nafasi ya kuwa Kiongozi.
No comments
Post a Comment