Zinazobamba

WAGOMBEA UDIWANI ILALA WAASWA KUVUNJA MAKUNDI.


Na Mussa Augustine.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Chief Sylvester Yaredi amewaomba Wagombea wa Udiwani Kata zote waliyoteuliwa kugombea nafasi hiyo Wilayani humo,wakawe sehemu ya kuvunja makundi kati yao na kamati za siasa za kata,nakuondoa tofauti walizo nazo ili waingie kwenye uchaguzi wakiwa wamoja. 

Yared amewaasa Madiwani hao leo August 15,2025 wakati akiwakabidhi barua za uteuzi wa kugombea nafasi hiyo,nakuwasisitiza kuwa wamoja ili kukisaidia Chama Cha Mapinduzi kupata Ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi Mkuu Oktoba 29,2025.

"Nimewatoa wasiwasi kuwa chama Cha Mapinduzi kimetumia Vigezo Mbalimbali ambapo kimebaini wanastahili na kufaa kugombea nafasi ya udiwani,walikua wagombea wengi lakini nafasi ilikua ni moja kwa maana hiyo waliopata nafasi ya uteuzi nimewaasa wasijione wao ni bora zaidi kuliko wenzao."

Nakuongeza" Cha pili ambacho nimewaasa wagombea wote wa Chama Cha Mapinduzi nafasi ya udiwani Wilaya ya Ilala,nimewaomba warudi chini wakajishushe kwa wale waliogombea nao na wanachama,wasipandishe mabega na kujiona wao ni wajanja sana kwa nafasi waliyoteuliwa bali ni nafasi ambayo imewangukia wao kwa wakati huu. 

Aidha Yared amesema kuwa Wagombea hao wamekiri pasina shaka watakua bega kwa bega na viongozi wenzao,na wanakwenda kuvunja makundi,kuongoe na wapambe wao,na wafuasi wao, namna ya kuacha kurushiana maneno ya kejeri bali wataenda kukaa nakuunganisha timu zote ili chama Cha Mapinduzi kitoke kikiwa umoja kuanzia kwenye mchakato mzima wa kampeni za Uchaguzi ambazo zinatarajiwa kuanza August 28,Mwaka huu.

No comments